KAIMU Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Bw.Nokta Banteze,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mafanikio na Mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 27,2025,katika Ofisi za Idara ya Habari-MAELEZO,jijini Dodoma.
SEHEMU ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Bw.Nokta Banteze (hayupo pichani) wakati akiwasilisha Mafanikio na Mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 27,2025,katika Ofisi za Idara ya Habari-MAELEZO,jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inatarajia kujenga maabara ya kisasa katika mkoa wa Dodoma kwa ajili kuimarisha uchunguzi wa sampuli za madini nchini ili kuchochea shughuli za utafiti nchini na hivyo kuhamasisha ukuaji wa Sekta ya Madini.
Hayo yameelezwa leo Machi 27,2025 na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Bw.Nokta Banteze,wakati akitoa taarifa ya mafanikio na Mwelekeo wa Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Ofisi za Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma.
“Maabara hiyo itakuwa na vifaa vya kisasa na itaweza kufanya uchunguzi wa sampuli za madini nyingi zaidi ikiwemo zinazojumuisha madini ya kimkakati na madini muhimu”amesema Bw.Banteze
Pia amesema GST imeshuhudia mageuzi na maboresho makubwa katika utoaji wa huduma zake na utendaji kazi wake kwa ujumla.
“Mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali pamoja na utayari wa viongozi wetu kuona GST inaimarika zaidi kwa ukuaji endelevu wa Sekta ya Madini.”amesema
Hata hivyo amesema kuwa GST kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekamilisha utafiti na uchoraji wa ramani ya jiolojia ya visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba).
Ambapo amesema kuwa visiwa vya Zanzibar havijawai kufanyiwa utafiti huo wa jiolojia..
“Matokeo ya utafiti huo yamebaini uwepo wa miamba ya chokaa yenye ubora wa kutengeneza saruji, Madini tembo, Madini ya silica, strontium, vyanzo vya maji ardhi, maeneo yenye vivutio vya utalii wa jiolojia na maeneo hatarishi kwa majanga ya asili ya jiolojia. “amesema Bw.Banteze
Aidha amesema kuwa uchukuaji wa sampuli za mchanga wa bahari kwa ajili ya kuchunguzi madini tembo katika Kisiwa cha Unguja na Pemba