Kamishna wa Idara Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, akiagana na Balozi wa Denmark Nchini, Mhe. Jepser Kammersgaar, baada ya kukamilika kwa mazungumzo yaliyolenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine (katikati), akiongoza kikao cha Wizara ya Fedha na Ujumbe wa Denmark, katika mazungumzo yaliyolenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bi. Tiba Kisonga na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melckzedeck Mbise na kulia ni Mchumi Mcumi kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Amosi Kambo na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Betha Mturi.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, akisalimiana na Balozi wa Denmark Nchini, Mhe. Jepser Kammersgaar, alipowasili na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo yaliyolenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Mfuko wa Danish Public Investment Fund for Development Countries (IFU), anayeshughulikia masuala ya Dhamana, Bw. Theo Ib Larsen.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Denmark Nchini, Mhe. Jepser Kammersgaar, alipowasili na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo yaliyolenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Balozi wa Denmark Nchini, Mhe. Jepser Kammersgaar, akizungumza wakati wa kikao na Wizara ya Fedha, alipowasili na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo yaliyolenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melckzedeck Mbise, akifafanua jambo wakati wa kikao na ujumbe wa Denmark, kilicholenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati, kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Danish Public Investment Fund for Development Countries (IFU), anayeshughulikia Sekta ya Umma katika Mikopo Nafuu na Misaada, Bi. Tina Kollerup Hansen, akifafanua jambo wakati wa kikao na Wizara ya Fedha, kilicholenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Mfuko wa Danish Public Investment Fund for Development Countries (IFU), anayeshughulikia masuala ya Dhamana Bw. Theo Ib Larsen, akifafanua jambo wakati wa kikao na Wizara ya Fedha, kilicholenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati, kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu – El Maamry Mwamba, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Danish Public Investment Fund for Development Countries (IFU), ukiongozwa na Balozi wa Denmark Nchini, Mhe. Jepser Kammersgaar, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.
Mazungumzo yao yalilenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati.
Aidha, kupitia Mfuko huo Tanzania inaweza kunufaika na aina mbalimbali za ufadhili unaotolewa na Mfuko huo ikiwemo uwekezaji wa hisa (equity investment), na dhamana (guarantees).
Kikao hicho kilihudhuriwa na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa IFU, anayeshughulikia Sekta ya Umma katika Mikopo Nafuu na Misaada, Bi. Tina Kollerup Hansen, na Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Dhamana, Bw. Theo Ib Larsen.
Kwa upande wa Wizara ya Fedha kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melckzedeck Mbise na Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bi. Tiba Kisonga.