Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule
akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.
Na Gideon Gregory, Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewahimiza wakina mama wa kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanajifunza kwa makini na kuwa tayari kupokea mafunzo watakayopatiwa na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) kwani yatawasaida kwenda kuajiliwa na kuwa watumishi bora.
Senyamule ameyasema hayo leo Machi 24,2025 Jijini Dodoma wakati akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya wanawake hao na kuongeza kuwa watakuwa watumishi bora kwasababu wametoka kwenye mafunzo ya VETA yenye ujuzi na utaalamu wa ufundi wanaoufanyia kazi.
“Mimi nina imani kuwa mafunzo haya yatakwenda kuleta mapinduzi katika sekta ya huduma hizo mnazojiajili ndani ya mkoa wa Dodoma, hivyo nitoe pongezi kwa Mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Dodoma kwani anafanya kazi nzuri sana na ndiye amefanikisha hili kwa juhudi zake anazozifanya,”amesema.
Aidha amesema kuwa wanawake wengi hawana ujuzi ndiyo maana hata kujiajili ili watoe huduma mbalimbali imekuwa changamoto pia hawana mitaji jambo linalopelekea wakipewa tenda za kazi kutatamani kukimbia.
“Unaweza ukampa tenda akasema napata wapi mtaji wa kutoa hiyo tenda, lakini bado kuna suala la nidhamu ya kazi yeye anajua pia akipata kazi anaifanyaje,”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore amesema katika mafunzo wanayoyatoa eneo waliloliwekea mkazo ni kuhakikisha wanawake wanaodahiliwa katika vyuo vya ufundi stadi wanaongezeka hadi kufikia 45% .
“Sasa hivi tunapata changamoto tuko 27% kunamuda tunakuwa hapo tunafika 35% lakini lengo letu tunataka tufike 45% wawe ni wanawake na kuweza kufikia haya tunayo mafunzo mbalimbali ambayo tunahitaji tuweze kuyafanya ili kuhakikisha sasa eneo hili la kufikia asilimia hizo tunazifikia,”amesema.
Awali Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma Deodatus Orotha amesema dhumuni la kuandaa mafunzo hayo ni kuwapatia ujuzi wanawake wa Mkoa wa Dodoma ili waweze kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii yao pamoja na familia zao na hivyo kuleta tija kwa taifa.
“Lengo ni kuwafikia wanawake wa Mkoa wa Dodoma wapatao 3000 na hivyo utaratibu utakuwa kwa hawamu na kwa kuanza tutaanza na wanawake 250 watakapomaliza watakuja wengine 250 mpaka tuweze kufikia idadi yetu ya mwisho tuliyoilenga,”amesema.
Naye Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Bi. Fatuma Madidi amesema wamefurahia fursa hiyo na wako tayari kujifunza hivyo wanaamini kupitia mafunzo hayo wataenda kuwa bora, wajuzi na kuongeza kipato na hali ya wanwake kuonekana ombaomba inakwenda kuondoka.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule
akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.
Mkuu ww Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma Deodatus Orotha akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.
Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Bi. Fatuma Madidi akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.
Wanawake wa kikundi cha wanawake na Samia mkoa wa Dodoma kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi chao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.
Picha ya pamoja ya washiriki wa ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.