Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Japhet Hasunga ( katikati) akiongoza wajumbe wa kamati ya Bunge katika kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
………..
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeipongeza Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa matumizi sahihi ya FORCE akaunti yenye kuleta tija kwenye miradi mbalimbali nchini.
Pongezi hizo zilitolewa Machi 24, 2025 Jijini Arusha, na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Japhet Hasunga mara baada ya kamati kukagua ujenzi wa mradi wa mabweni ya wanafunzi.
Aidha Kamati hiyo pia imepongeza NM-AIST kwa kuzalisha bunifu110 huku bunifu 22 zikipata hati miliki na kusisitiza bunifu hizo kubishwarishwa ili kuleta tija zaidi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi nyingine zinazofika kujifunza kuhusu masuala ya bunifu.
Vilevile, kamati hiyo imeiagiza NM-AIST kuhakikisha inaendelea kufanya bunifu ikiwemo kuzisajili kwa kupata hati miliki ili kuepuka Teknolojia hizo kuibiwa zinazogunduliwa na wabunifu.
Mhe. Hasunga alisema, endapo bunifu hizo zikitoa matokeo ya bunifu upatikanaji wa hati miliki utasaidia wabunifu kutoibiwa mawazo yao sanjari na kuziuza ili wahusika waweze kupata kipato na kujikwamua kiuchumi.
“Bunifu zenu hakikisheni zinaingia sokoni lakini pia tunawapongeza kwa muonekano wa thamani halisi ya fedha za mradi huu ikiwemo matumizi ya force akaunti” Mhe.Hasunga
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Profesa Maulilio Kipanyula ambaye ni Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, alisema jengo hilo la mabweni pacha matatu lina thamani ya sh bilioni 6.109 likiwa na vyumba 184 ambapo vyumba 160 ni vya kujitosheleza na vyumba 20 ni vya mfano wa apatimenti kwa ajili ya kinamama wenye watoto pamoja na vyumba vinne kwa ajili ya matumizi mtambuka.
Prof Kipanyula alisema mradi huo wa mabweni pacha matatu umefikia asilimia 74 na unatarajia kukamilika Juni 30, 2025 ambapo lengo kuu la taasisi hiyo, ni kutoa mafunzo ikiwemo utafiti ambapo hadi sasa kuna wanafunzi kutoka nchi 16 tofauti za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa j Nangwa la Sahara wanasoma katika taasisi hiyo.
Kuhusu ufafanuzi wa bunifu ya inzi lishe , Naibu Makamu Mkuu ,Taaluma,Utafiti na Ubunifu Profesa Anthony Mshandete alisema inzi chuma huyo ni nzi asiyeambukiza na hutaga mayai zaidi ya 500 ambayo huzilisha funza lishe kwa ajili ya kutengeneze chakula cha mifugo na mbolea.
Alisema uzalishaji wake unajali mazingira ikiwemo uchafu unaozalishwa na zao la mkonge kubuniwa na hatimaye kupata chakula hicho cha mifugo na mbolea rafiki kwa wakulima.
Awali wabunge wa kamati hiyo akiwemo, Mhe. Isack Kamwelwe mbunge wa Katavi na Mhe. Condester Sichalwe kutoka Momba walipongeza taasisi hiyo, kwa kufanya bunifu mbalimbali na ufanisi wa mradi wa bweni hilo ikiwemo mandhari nzuri ya taasisi hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Japhet Hasunga akizungumza wakati wa kikao mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ( Hosteli) unaotekelezwa na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akiongea jambo wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) iliyofanya ziara ya kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Balozi Maimuna Tarish akizungumza wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) waliofanya ziara ya kukagua na kutembelea mradi wa ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wa Taasisi hiyo, Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa mabweni ya wanafunzi kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) , Machi 25,2025 kampasi ya Tengeru Jijini Arusha.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Japhet Hasunga ( katikati) akiongoza wajumbe wa kamati ya Bunge katika kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi Prof. Kelvin Mtei ( katikati) akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) walipotembelea mradi huo katikati Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) iliyofanya ziara ya kutembelea na kukagua Mradi huo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakifuatilia wasilisho la taarifa ya utekelezaji wa mradi wa bweni la wanafunzi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( hayupo katika picha) Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Wajumbe wa Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) wakiwa katika cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mara baada ya ziara ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.