Featured Kitaifa

BENKI YA USHIRIKA YATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA USHIRIKA KUJIENDESHA KIBIASHARA

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma. 

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Abdulmajid Nsekela ametoa wito kwa Benki ya Ushirika kutumia fursa za Ushirika kuongeza tija kibiashara kwa Benki hiyo.

Amesema hayo wakati Kamisheni ya Tume ilipofanya ziara ya kutembelea na kujifunza hatua za kiutendaji zilizofikiwa na Benki hiyo Machi 25, 2025 Jijini Dodoma.

Amesema ni muhimu Benki hiyo kuangalia namna bora ya kutumia Vyama vya Ushirika katika kuongeza fursa za wateja, biashara na mikopo yenye ushindani kwa Vyama.

Akieleza kuhusu Benki hiyo Mkurugenzi Mtendaji Godfrey Ng’urah amesema Benki hiyo tayari inafanya kazi na Vyama vya Ushirika kwa karibu na itaendelea kuunganisha Benki hiyo na Mifumo ya TEHAMA ili kutoa huduma kidijitali na kuwafikia wanachi wengi.

Kwa upande wake Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amesema Tume iko tayari kuendelea kutoa ushirikiano wakati wote ili kuhakikisha azma ya Serikali ya uanzishaji na uendeshaji wa Benki hiyo unafanyika kwa ufanisi.

Aidha, Kamisheni imetembelea Ofisi za Tume na kujadili masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuboresha Ushirika nchini.

About the author

mzalendo