Featured Kitaifa

WAFANYABIASHARA TUENDELEE KUWA NA IMANI NA RAIS SAMIA -MAJALIWA

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembelea Kiwanda cha Kusindika  Mafuta ya Parachichi cha AvoAfrica Tanzania Limited kilichopo wilaya ya Wanging’ombe mkoani Lindi Machi 23, 2025. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana, kulia   ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exhaud Kigahe, wa tatu kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI na Mbunge wa Wanging’ombe, Dkt. Festo Dugange na kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Nagib Kamal. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

….

 

Ampongeza Kamishna TRA kwa kusimamia Weledi patika ukusanyaji wa kodi

-Atembelea kiwanda cha uchakataji mazao ya parachichi

WAZIRI MKUU,  Kassim Majaliwa amezitaka jumuiya za wafanyabiashara nchini kuendelea kuwa na imani na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amedhamiria kutatua changamoto zinazohusu masuala ya kodi.

Amesema Rais Dkt. Samia anajali changamoto za wafanyabiashara na ndio maana ameunda timu mbalimbali kwa ajili ya kufanya mapitio ya kero za wafanyabiashara wafanye kazi zao kwa uhuru.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo leo (Jumapili 23 Machi 2025) alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa na Mwakilishi wa wafanyabiashara wa Halmashauri ya Makambako aliposimama na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.

“Nataka niwatoe Mashaka Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan baada ya mapendekezo yenu wafanyabiashara yale kumi na tano, kufuatia mkutano na wafanyabiashara Kariakoo ameunda tume inayofanya mapitio ya mfumo wa kodi Tanzania na inaendelea kuzunguka nchi nzima kufanya kazi hiyo.” 

Aidha, amempongeza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato nchini sambamba na kuchukua hatua kwa watendaji wa Mamlaka hiyo ambao wanaenda kinyume na maadili yao ya kazi.

Pia amemtaka kamishna huyo kuendelea kuboresha programu za utoaji wa elimu kwa mlipa kodi, ili kuondoa changamoto zinazowakabili wafanya biashara kuhusu masuala ya kodi.

“Serikali hii inamtaka kila mtanzania ajue umuhimu wa kulipa kodi na tunajua kuwa sasa watanzania wengi wanajua umuhimu wa kulipa kodi.”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametembelea kiwanda cha uchakataji zao la parachichi cha Avo Afrika, kilichopo Mkoani Njombe.

Akizungumza na wafanyakazi na baadhi ya wananchi wanaouza bidhaa zao katika kiwanda hicho, Mheshimiwa majaliwa ametoa wito kwa wakulima wa zao la parachichi kuendelea kulima zao hilo kwani sasa zao hilo lina soko la uhakika.

“Nataka niwaambie sasa hali imebadilika parachichi ni biashara tosha, kama unataka utajiri lima parachichi, ukilima leo una uhakika wa mahali pa kuuza kwa sababu sasa wawekezaji wa uhakika wapo.”

Pia, Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka kwa kulifanya zao la parachichi kuwa ajenda ya uchumi mkoani humo pamoja na kuhakikisha zao hilo linapata soko la uhakika. 

Amesema Serikali imetoa maelekezo thabiti juu ya usimamizi wa mazao ya kilimo parachichi likiwemo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama parachichi alipotembelea Kiwanda cha Kuchakata  zao la  Parachichi  AvoAfrica Tanzania Limited kiichopo Makambako Mkoani Njombe, Machi 23, 2025. Kulia kwake ni Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Nagib Kamal. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Nagib Kamal  ambaye ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kuchakata Parachichi cha AvoAfrica Tanzania Limited kilichopo Makamabako Mkoa wa Njombe  kuhusu makasha yenye parachichi  yanayosubiri kusafirishwa nje ya nchi, Machi 23, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuchakata Parachichi cha AvoAfrica Tanzania Liited,  Nagib Kamal (kulia) kuhusu  uchakataji wa Parachichi, Machi 23, 2025. Wa pili kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana na kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exhaud Kigahe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Nagib Kamal, Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kusindika  Mafuta ya Parachichi cha AvoAfrica Tanzania Limited killichopo  wilaya  ya Wanging’ombe Mkoani Njombe, Machi 23, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembelea Kiwanda cha Kusindika  Mafuta ya Parachichi cha AvoAfrica Tanzania Limited kilichopo wilaya ya Wanging’ombe mkoani Lindi Machi 23, 2025. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana, kulia   ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exhaud Kigahe, wa tatu kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI na Mbunge wa Wanging’ombe, Dkt. Festo Dugange na kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Nagib Kamal. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Kiwanda cha Kusindika Mafuta ya  Parachichi cha AvoAfrica Tanzania Limited  alipotembelea kiwanda hicho kilichopo wilyani Wanging’ombe mkoa wa Njombe Machi 23, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana viongozi wa Mkoa wa Njombe kwenye Kiwanda cha Kukamua Mafuta ya Parachichi cha AvoAfrica Tanzania Limited kilichopo wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe Machi 23, 2025. Kulia ni Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Nagib Kamal. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

mzalendoeditor