Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MSIBA WA BI. DAMARIS HAWASSI

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiwa na Katibu wa NEC (Uchumi na Fedha) wa Chama Cha Mapinduzi  Dkt. Frank Hawassi kufuatia kifo cha Mke wake Bi. Damaris Hawassi ambaye ni mke wa Dkt. Frank Hawassi wakati alipowasili kushiriki msiba huo Miyuji Jijini Dodoma tarehe 21 Machi 2025.

….

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameshiriki msiba wa Bi. Damaris Hawassi ambaye ni Mke wa Katibu wa NEC (Uchumi na Fedha) wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Frank Hawassi katika makazi ya familia hiyo mtaa wa Miyuji Jijini Dodoma.

Akiwafariji waombolezaji katika msiba huo, Makamu wa Rais ametoa salamu za rambirambi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa pole sana kwa familia na waombolezaji wote kufuatia msiba huo. 

Makamu wa Rais amewaombea faraja wanafamilia pamoja na wote walioguswa na msiba huo. Amewashukuru wananchi waliojitokeza kuifariji familia katika kipindi hiki kigumu kwao.  

Makamu wa Rais amesema ni vema Watanzania kuendelea kushirikiana katika changamoto mbalimbali zinapotokea katika jamii ikiwemo magonjwa na vifo kwa kudumisha undugu, amani na kupendana ili kuwa na Taifa zuri na lenye ustawi. 

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema Bi.Damaris Hawassi alikua mchapakazi hodari aliyetimiza vema wajibu wake  katika umri aliyojaaliwa duniani.  Ameongeza kwamba ni vema kujifunza juu ya kila mmoja kutimiza wajibu wake pamoja na kuishi vema na wanadamu wengine. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Katibu wa NEC (Uchumi na Fedha) wa Chama Cha Mapinduzi  Dkt. Frank Hawassi kufuatia kifo cha Mke wake Bi. Damaris Hawassi wakati alipowasili kushiriki msiba huo Miyuji Jijini Dodoma tarehe 21 Machi 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiwa na Katibu wa NEC (Uchumi na Fedha) wa Chama Cha Mapinduzi  Dkt. Frank Hawassi kufuatia kifo cha Mke wake Bi. Damaris Hawassi ambaye ni mke wa Dkt. Frank Hawassi wakati alipowasili kushiriki msiba huo Miyuji Jijini Dodoma tarehe 21 Machi 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na akiwa na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Bi. Damaris Hawassi ambaye ni Mke wa Katibu wa NEC (Uchumi na Fedha) wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Frank Hawassi wakati walipowasili kushiriki msiba huo Miyuji Jijini Dodoma tarehe 21 Machi 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na akiwa na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiwafariji waombolezaji mbalimbali waliojitokeza kushiriki msiba wa Bi. Damaris Hawassi ambaye ni Mke wa Katibu wa NEC (Uchumi na Fedha) wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Frank Hawassi Miyuji Jijini Dodoma tarehe 21 Machi 2025.

About the author

mzalendoeditor