AFISA Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki (COSOTA) Bi.Doreen Anthony Sinare,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Machi 21, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIKA kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita, kutokana na mafunzi COSOTA imetoa jumla ya vyeti 7,679 vya uthibitisho wa umiliki wa hakimiliki kwa wabunifu waliosajili kazi zao.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki (COSOTA) Bi.Doreen Anthony Sinare,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Machi 21, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.
Bi.Sinare amesema kuwa usajili wa kazi zinazolindwa na Sheria ya hakimiliki na hakishiriki umeongezeka kwa asilimia 70 Ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kuanzia mwaka 2021 mpaka Februari 2025,
“COSOTA imesajili kazi za Sanaa na uandishi 11,519 na Wabunifu 3,436. Idadi hiyo ya wabunifu pamoja na kazi zao imetokana na zoezi la utoaji wa elimu na mafunzo mbalimbali ya hakimiliki na usajili kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, semina lakini pia kushiriki matukio mbalimbali ya wadau”amesema Bi.Sinare
Aidha Bi.Sinare amesema kuwa COSOTA ilipata fursa ya kuelimisha wadau kuhusiana na hakimiliki na uhamasishaji wa usajili wa kazi za hakimiliki.
Amesema katika kipindi hicho kamati maalumu ya Usajili ndani ya COSOTA inayojihusisha na masuala ya usajili, imefanikiwa kutoa mafunzo na ufafanuzi kuhusiana na hakimiliki kwenye kazi zilizopokelewa katika kipindi hicho kwa idadi ya wabunifu 167.
Hata hivyo amesema katika kipindi cha Miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan COSOTA imefanikiwa kupokea jumla ya migogoro 136.
Amesema Kati ya Migogoro hiyo Migogoro 118 imetatuliwa, migogoro 10 haijafanyiwa kazi bado na Migogoro 8 bado inafanyiwa kazi.