Featured Kitaifa

EWURA YAPOKEA MAONI YA WADAU KUHUSU UBORA WA HUDUMA

Written by mzalendoeditor
Sehemua ya  washiriki kutoka Mamlaka za Maji wakifatilia  mkutano wa wadau uliondaliwa na  EWURA kujadili maboresho ya Kanuni za Utoaji huduma za maji nchini,leo Machi 20,2025  jijini Dar es Salaam.
Na.Mwandishi Wetu-Dar es Salaam:
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo, 21 Machi 2015, imekutana na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kwa lengo la kupokea na kujadili maoni kuhusu maboresho ya  Kanuni za Ubora wa Huduma ya Maji ili kuongeza ufanisi kwa Mamlaka hizo katika kuwahudumia wateja wake.
Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA, Mhandisi Exaudi Maro,  alibainisha kuwa baadhi ya maboresho ya Kanuni hizo ni pamoja na  mapendekezo ya kuongezeka muda wa kutumika bei za maji kutoka miaka mitatu ya sasa hadi mitano, kuboresha muda wa kuwasilisha taarifa za utendaji, na kuweka ukomo wa mipango ya kibiashara ya mamlaka za maji.
Sabina Faya, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mha. Mwajuma Waziri, aliwasisitiza washiriki kutoa maoni yenye tija ili yawe na matokeo chanya katika kuboresha huduma na kuongeza ufanisi wa huduma ya maji kwa wateja nchini.

Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Exaudi Maro,akizungumza wakati wa Mkutano wa wadau wa Mamlaka za Maji  uliondaliwa na  EWURA kujadili maboresho ya Kanuni za Utoaji huduma za maji nchini,leo Machi 20,2025  jijini Dar es Salaam.

Sehemua ya  washiriki kutoka Mamlaka za Maji wakifatilia  mkutano wa wadau uliondaliwa na  EWURA kujadili maboresho ya Kanuni za Utoaji huduma za maji nchini,leo Machi 20,2025  jijini Dar es Salaam.

Sehemua ya  washiriki kutoka Mamlaka za Maji wakifatilia  mkutano wa wadau uliondaliwa na  EWURA kujadili maboresho ya Kanuni za Utoaji huduma za maji nchini,leo Machi 20,2025  jijini Dar es Salaam.

About the author

mzalendoeditor