Featured Kitaifa

DKT.JINGU ATETA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA KIMATAIFA WA WANAWAKE NA AMANI JIJINI NEW YORK MAREKANI

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa mtandao wa kimataifa wa wanawake na amani (Internationsl Women Peace Group ambao makao yake makuu yapo nchini korea). Kikao hicho kilifanyikia Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.

Katika kikao hicho IWPG ilieleza shughuli inazotekeleza nchini Tanzania katika mikoa ya Arusha, Njombe na Dar Es Salaam ikihusisha elimu ya amani kwa watoto kupitia uchoraji ambapo uendesha mashindano ya uchoraji . Vilevile alieleza nia ya IWPG kushirikiana na Serikali katika kufikia mikoa yote kutekeleza mpango huo.

Dkt. Jingu aliushukuru mtandao huo kwa jitihada zake na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao.

About the author

mzalendoeditor