Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati akizindua Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2023/24,hafla iliyofanyika leo Machi 19,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa jitihada zake katika kusimamia Sekta ya Maji. Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na EWURA ili kuhakikisha huduma za maji kwa wananchi zinaimarika.
Dkt. Biteko alitoa pongezi hizo leo, Jumatano tarehe 19 Machi 2025, wakati akizindua Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia matokeo ya ripoti hiyo, Dkt. Biteko alibainisha mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Maji, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa maji kwa asilimia 7, kutoka mita za ujazo milioni 593 mwaka 2022/2023 hadi mita za ujazo milioni 685 mwaka 2023/2024.
Aidha, maunganisho ya huduma za maji yaliongezeka kwa asilimia 9, kutoka kaya 1,532,362 mwaka 2022/2023 hadi kaya 1,669,298 mwaka 2023/2024.
“Ripoti hii pia imeonesha ongezeko la ufungaji wa mita za maji kwa asilimia 2, kutoka mita 1,444,874 mwaka 2022/2023 hadi mita 1,581,418 mwaka 2023/2024, hatua inayolenga kuboresha usimamizi wa matumizi ya maji,” aliongeza.
Hata hivyo, Dkt. Biteko alitaja changamoto zinazoikabili sekta hiyo, kuwa ni uzalishaji wa maji usiokidhi mahitaji ya wananchi, upotevu wa maji wa asilimia 36 ambao ni juu ya kiwango kinachokubalika cha asilimia 20, ukosefu wa huduma bora za usafi wa mazingira, na gharama kubwa za uendeshaji zinazotokana na upotevu wa maji na miundombinu duni ya kutibu maji na majitaka.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika kudhibiti upotevu wa maji ili kuboresha huduma na kuongeza ufanisi katika sekta ya maji nchini.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam kuzindua taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za maji kwa mwaka 2023/24.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati akizindua Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2023/24,hafla iliyofanyika leo Machi 19,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2023/24,hafla iliyofanyika leo Machi 19,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Profesa Mark Mwandosya,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2023/24,hafla iliyofanyika leo Machi 19,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt. James Andelile,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2023/24,hafla iliyofanyika leo Machi 19,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko,akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa EWURA mara baada ya kuzindua Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2023/24,hafla iliyofanyika leo Machi 19,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.