Walimu 646 wa Shule za Msingi Wanufaika na Mafunzo yanayolenga kuwezesha utekelezaji wa Mpango wa Shule Salama kwa Shule za Awali na Msingi ili kumwezesha mwanafunzi kusoma na kumaliza mzunguko wake wa Elimu.
Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Serikali chini ya ufadhili wa Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania (BOOST).
Walimu hao ni wa shule za Msingi kutoka mikoa sita ambayo ni Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, na Ruvuma.
Mafunzo yameanza Machi, 18, 2025 katika Chuo cha Ualimu Klerruu, mkoani Iringa ambapo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia, pamoja na umoja wa wazazi na walimu (UWAWA).