Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI amempa mkandarasi anayejenga jengo la TAMISEMI katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma miezi miwili kuhakikisha anakamilisha ujenzi, ili ifikapo Juni Mosi mwaka huu jengo hilo lianze kutumika rasmi.
Waziri Mchengerwa ametoa agizo hilo jijini Dodoma alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo leo tarehe 14.03.2025.
Mhe. Mchengerwa amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha kazi inafanyika kwa ufanisi usiku na mchana bila visingizio vyovyote.
Kwa upande wake, Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kutoka Vikosi vya Ujenzi, Mhandisi Deogratius Japhet, ameahidi kutekeleza agizo hilo na kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.