Featured Magazeti

DKT. NCHEMBA ASHIRIKI MKUTANO WA 50 WA BODI YA WADHAMINI YA BENKI YA EADB

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akisalimiana na Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Ng’ongo John Mbadi, wakati walipokutana katika Mkutano wa 50 wa Bodi ya Wadhamini (Governing Council) ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), uliofanyika tarehe 13 Machi 2025, katika Hoteli ya Serena, jijini Kampala-Uganda. Mkutano huo uliwashirikisha Wadhamini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Tanzania, Dkt. Charles Mwamwaja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Benard Mono.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akisalimiana na kufurahi na Waziri wa Fedha wa Uganda, Mhe. Matia Kasaija, wakati walipokutana katika Mkutano wa 50 wa Bodi ya Wadhamini (Governing Council) ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), uliofanyika tarehe 13 Machi 2025, katika Hoteli ya Serena, jijini Kampala-Uganda. Mkutano huo uliwashirikisha Wadhamini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Tanzania, Dkt. Charles Mwamwaja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Benard Mono.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa kwanza kushoto), na Mawaziri wenzake wa Fedha, Mhe. Matia Kasaija (Uganda) (wa pili kushoto), Mhe. Ng’ongo John Mbadi (Kenya)(wa kwanza kulia) na Mhe. Yusuf Murangwa (Rwanda)(wa pili kulia), wakiteta jambo wakati walipokutana kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 50 wa Bodi ya Wadhamini (Governing Council) ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), unaofanyika leo tarehe 13 Machi 2025, katika Hoteli ya Serena, jijini Kampala-Uganda. Mkutano huo uliwashirikisha Wadhamini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Tanzania, Dkt. Charles Mwamwaja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Benard Mono. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Kampala-Uganda)

About the author

mzalendoeditor