Mifugo aina ya ng’ombe inayopatikana kwenye mashamba ya kuzalishia Mifugo na Malisho ya Ranchi za Taifa Usangu wakati wa Ziara yake Machi 7, 2025 Wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti akizungmza na wawekezaji na wafugaji katika mashamba ya kuzalishia Mifugo na Malisho kwenye Ranchi za Taifa Usangu wakati wa Ziara yake Machi 7, 2025 Wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Bw. Mrida Mshota akizungumza wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti kukagua mashamba ya kuzalishia Mifugo na Malisho kwenye Ranchi za Taifa Usangu wakati wa Ziara yake Machi 7, 2025 Wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Wafugaji na Wawekezaji wakimsikiliza Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti akitoa msimamo wa serikali kuhusu mashamba ya serikali ya kuzalishia Mifugo na Malisho kwenye Ranchi za Taifa Usangu wakati wa ziara yake Machi 7, 2025 Wilayani Mbarali mkoani Mbeya.Mhe.Mnyeti ametoa maelekezo hayo Machi 7, 2025 Wilayani MbeyaΒ wakati wa Ziara yake Kwenye Ranchi ya Usangu ambapo amesema serikali imetoa mashamba hayo kwaajili kuzalishia mifugo na sio shughuli za Kilimo.
” Mashamba haya ni ya kwaajili ya MifugoΒ lakini kuna watu walikuja kutaka kukodisha kwaajili ya kuzalisha mifugo lakini wamegeuza matumizi na sasa wanalima hili halikubaliki, Nawapa siku tatu Narco kuwaandikia notisi wote waliokiuka”alisema Mhe. Mnyeti.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) Bw. Mrida MshotaΒ amesema ili kuweza kunufaika na sekta ya mifugo lazima jamii ya wafugaji na wawekezaji kukubaliana na mabadiliko.
Ziara ya Mhe. Mnyeti itaendelea kesho kwa mkoa wa Rukwa

