Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Wanawake watumishi kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzani wameshiriki maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Chinangari Park Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya maadhimisho hayo leo Machi 8,2025 Afisa Ugavi wa Tume hiyo Bi. Aneth Lyatuu amesema kuwa siku ya leo inawakumbusha na kuwapa ujasili zaidi wa kuweza kusimamia malengo ambayo wamejiwekea katika akili zao.
“Siku ya leo niwaambie wanawake wenzangu tujitahidi kupendana mwenzako akikukasilisha mwambie, msamehe na tusonge mbele pia tutiane moyo na nguvu,”amesema.
Aidha amesema kupitia maadhimisho hayo wanawake wasisahahu maadili ya watoto kwasababu wanawake ndiyo wanaoongoza jamii na inaanzia katika familia na wakisimama imara jamii yote itaimalika.
Maadhimisho ya siku ya Wanamke Duniani kitaifa yamefanyika Jijini Arusha ambapo yameongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.