Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza wakati wa Kikao kazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kikao hicho kilishirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na maafisa bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akipitia nyaraka na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. John Cheyo, akichukua taarifa wakati wa Kikao kazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kikao hicho kilishirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na maafisa bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Makamishna Wasaidizi wa Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Bi. Bahati Mgongolwa (kushoto), Bi. Vicky Jengo na Bw. Andambike Mololo, wakifuatilia kwa karibu Kikao kazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kikao hicho kilishirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na maafisa bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Kikao kazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, wakifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa katika Kikao kazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kilichowashirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na maafisa bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary akizungumza katika Kikao kazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kikao hicho kilishirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na maafisa bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Dodoma)
Na. Scola Malinga, WF, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, amefungua Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kinachoshirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
Kikao kazi hicho kimelenga kufanya uchambuzi wa bajeti ili kuwa na uelewa wa pamoja wa jinsi mipango na rasilimali fedha zinavyoelekezezwa katika afua/maeneo ya kimkakati ili kuwezesha Serikali kufikia malengo ya muda mfupi, wa kati na mrefu kama ilivyoainishwa katika Mwongozo wa Mpango na Bajeti wa Mwaka 2025/26, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III) pamoja na Sera na vipaumbele vya Kisekta.
Aidha, uchambuzi unalenga kuongeza ushirikiano (synergies) katika utekelezaji wa mipango kati ya Sekta zinazotegemeana.