Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utiaji Saini wa makubalino ya kisiasa mkutano uliofanyika tarehe 5 Machi, 2025 Maputo, Msumbiji.
Katika kikao hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alialikwa kwa nafasi yake ya Uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kuhudhuria hafla ya utiaji Saini wa makubaliano ya kisiasa kuhusu majadiliano Jumuishi ya Kitaifa kutafuta suluhu ya kudumu kufuatia uhasama baina ya wadau wa Kisiasa nchini humo uliojitokeza mara baada ya Uchaguzi Mkuu
Hafla hiyo ni sehemu ya mchakato wa ndani wa mageuzi ya kisiasa yanayolenga kufanikisha mjadala wa pamoja ili kufikia muafaka wa Kitaifa kufuatia hali ya kisiasa na usalama iliyojitokeza Nchini Msumbiji baada ya Uchaguzi Mkuu wa Nchi hiyo uliofanyika tarehe 09 Oktoba, 2024