Featured Kitaifa

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Written by mzalendoeditor

WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,akiwa na Kamishna   wa maadili, Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi,(Kulia) na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka,(kushoto).

Na.Alex Sonna-DODOMA

CHUO  cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wameingia makubaliano ya kushirikiana kutoa mafunzo ya maadili kwa viongozi wa umma ili kuwa wadilifu na wasimamizi bora wa rasilimali.

Akizindua leo Machi 6,2025 jijini Dodoma makubaliano hayo,Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,amesema kuwa  serikali inaendelea kuchukua hatua thabiti kuhakikisha kuwa maadili yanazingatiwa kwa kuimarisha sheria, mifumo ya uwajibikaji, na mafunzo kwa viongozi wa umma.

Hata hivyo Mhe.Simbachawene,amehimiza taasisi zote za serikali kuhakikisha viongozi wake wanahudhuria mafunzo hayo ambayo yamegawanywa katika makundi 13 ya awali, yanayowalenga viongozi wa mashirika ya umma, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Idara, Maofisa wa Elimu na sekta nyingine muhimu.

“Kupitia mafunzo haya, tunatarajia kuwa viongozi wetu watakuwa na uelewa mpana wa misingi ya utawala bora na maadili katika utoaji wa huduma kwa umma,”amesema Mhe.Simbachawene

Kwa upande Kamishna wa maadili, Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi, amesema kuwa mafunzo hayo pia yatawajenga watumishi wa umma ili waepukane na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka .

Naye Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka, amesema  mafunzo hayo yanalenga kuwajengea viongozi wa umma ujuzi wa kina kuhusu maadili katika uongozi, utawala bora, matumizi ya fedha za umma, mifumo ya manunuzi, utoaji wa huduma kwa wananchi, na jinsi ya kutambua na kuondoa migogoro ya kimaslahi.

“Mafunzo hayo yatasaidia katika kutekeleza Mpango wa Taifa wa Kukuza Uadilifu (NACSAP), ambao unalenga kupunguza mianya ya rushwa na kuimarisha utawala wa sheria katika sekta ya umma.”amesema Prof. Sedoyeka

Awali,Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha Simbani Liganga,amesema kuwa  mafunzo hayo yatachangia kujenga utumishi katika sekta ya umma na binafsi kuongozwa na uadilifu, uwazi, na uwajibikaji.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,akizungumza  wakati akizindua makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

KAMISHNA  wa maadili, Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi,akizungumza  wakati wa uzinduzi wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka,akizungumza  wakati wa uzinduzi wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha Simbani Liganga,akizungumza  wakati wa uzinduzi wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

Makamu Mkuu wa Chuo, Mafunzo, Utafiti na Ushauri, Dk. Grace Temba,akizungumza  wakati wa uzinduzi wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,(hayupo pichani)   wakati wa uzinduzi wa  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,(hayupo pichani)   wakati wa uzinduzi wa  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,(hayupo pichani)   wakati wa uzinduzi wa  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,(hayupo pichani)   wakati wa uzinduzi wa  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,(hayupo pichani)   wakati wa uzinduzi wa  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,(hayupo pichani)   wakati wa uzinduzi wa  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,(hayupo pichani)   wakati wa uzinduzi wa  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,akiwa na Kamishna   wa maadili, Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi,(Kulia) na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka,(kushoto).

WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua  makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,hafla iliyofanyika leo Machi 6,2025 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor