Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia Prof. Carolyne Nombo amesema Serikali inasisitiza ushirikiano na wadau mbalimbali wa elimu katika kutekeza kwa ufanisi Sera mpya ya Elimu na mitaala ili kuwezesha maarifa, stadi na ujuzi stahiki kwa vijana waweze kuchangia katika kuleta maendeleo endelevu ya Taifa.
Prof. Nombo ameeleza hayo Februari 26, 2025 jijini Dodoma akifungua Mkutano wa Pamoja wa Tathimini ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu ambapo amesema nguvu kubwa inahitaji kwenye ujenzi wa miundombinu.
Miundombinu hiyo ni pamoja na madarasa na karakana upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ikiwemo vifaa vya mafunzo ya amali na TEHAMA na Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini.
Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa Serikali inaendelea na maandalizi ya zana za kuwezesha utekelezaji wa Sera ikiwemo miongozo, nyaraka, mapitio ya Sheria ya elimu na kuweka mifumo mbalimbali.