Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anorld Makombe (wa pili kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini imemtunuku Tuzo ya Heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake wa kipekee unaoonekana katika mafanikio ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Tuzo hii inakuja kama ishara ya kuthamini juhudi kubwa za Rais Samia katika kuleta maendeleo ya nchi, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati.
Pia, Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga Mjini inampongeza Rais Samia kwa kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais kwa kipindi cha 2025-2030 kupitia CCM, hatua inayothibitisha imani ya chama na wananchi kwa uongozi wake.
Tuzo hiyo imekabidhiwa leo Jumanne Februari 25,2025 wakati wa Kongamano kubwa la Kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais mwaka 2025 na makamu wake Dkt. Emmanuel Nchimbi lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini likiongozwa na kauli mbiu ‘Ushindi wa CCM 2025 Jumuiya ya Wazazi Tupo Mstari wa mbele’ likihudhuriwa na maelfu ya wanachama na viongozi wa CCM kutoka kata 17 za Jimbo la Shinyanga Mjini.

Akizungumza wakati akikabidhi tuzo hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko, amesema Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini imemtunuku Tuzo ya Heshima Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake uliotukuka wenye tija na mafanikio makubwa nchini kiuchumi, kisiasa na kijamii. Pia Jumuiya hiyo inampongeza Dkt. Samia kwa kuteuliwa kuwa mgombea nafasi ya Urais 2025-2030 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Wana Shinyanga tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Samia kutokana na mafanikio ya maendeleo ya wananchi ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo hivyo, tunampongeza Dkt. Samia kwa kuteuliwa kuwa mgombea nafasi ya Urais 2025-2030 kupitia CCM”,amesema.
Aidha amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani na mshikamano nchini kuelekea uchaguzi wa 2025, huku akitaka kila mmoja apinge vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuhimiza malezi bora kwa watoto na vijana.
Kwa niaba ya Rais Samia, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anorld Makombe, ameipokea tuzo hiyo na kusema, “Kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi, Rais Samia amefanya mambo makubwa. Kazi yake imetufanya tuwe na amani na utawala bora, na ndiyo maana CCM imemchagua kugombea Urais 2025.”
Viongozi mbalimbali wamewasilisha pongezi zao, wakiwemo Mfanyabiashara maarufu Gilitu Makula, ambaye amesisitiza umuhimu wa watanzania kuwa mabalozi wa mazuri yanayofanywa na Rais Samia, na Mchungaji Andrea Salu wa Kanisa la EAGT Ndala, ambaye amemtaja Rais Samia kama kiongozi shujaa anayeongoza kwa hekima.
“Sisi wafanyabiashara tunampongeza Mhe. Rais Samia kwa jinsi anavyozidi kufungua nchi .Anayemchukia Rais Samia ni chuki zake tu binafasi, wafanyabiashara hivi tuna amani, tunalipa kodi bilaaa kusumbuliwa, kwanini tusimpe hii mitano tena? . Tuwe mabalozi wa kuyasemea mazuri yanayofanywa na Rais Samia, vinginevyo ni hila tu za watu binafasi”,amesema Gilitu.
“Tuna rais Shujaa kabisa anatuongoza vizuri, kazi yetu viongozi wa dini ni kuiombea nchi yetu amani iendelee kudumu, tunazuia roho zote zinazotaka tumwage damu”,amesema Mchungaji Salu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko (kushoto) akimkabidhi tuzo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anorld Makombe, aliyeipokea kwa niaba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anorld Makombe (kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anorld Makombe (wa pili kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anorld Makombe akizungumza wakati akipokea tuzo kwa niaba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anorld Makombe akizungumza wakati akitoa tamko Wana CCM Shinyanga Mjini kuunga mkono maamuzi ya CCM kumpitisha Rais Samia kwa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais kwa kipindi cha 2025-2030 kupitia CCM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza wakati wa Kongamano la Kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais mwaka 2025 na makamu wake Dkt. Emmanuel Nchimbi lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anorld Makombe akizungumza wakati wa Kongamano la Kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais mwaka 2025 na makamu wake Dkt. Emmanuel Nchimbi lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Kibabi akizungumza wakati wa Kongamano hilo
Wanachama na viongozi wa CCM wakifanya matembezi wakati wa Kongamano la Kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais mwaka 2025 na makamu wake Dkt. Emmanuel Nchimbi lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini