Featured Kitaifa

MRINDOKO AZINDUA SHINA LA WAKEREKETWA LA WAJASIRIAMALI CHAMAGUHA, APOKEA WANACHAMA WAPYA 50 WAZAZI KOLANDOTO

Written by mzalendoeditor

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko akipandisha bendera ya CCM wakati akizindua Shina la Wakereketwa la Wajasiriamali katika tawi la Chamaguha, kata ya Chamaguha

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko, amezindua Shina la Wakereketwa la Wajasiriamali katika tawi la Chamaguha, kata ya Chamaguha, pamoja na kupokea wanachama wapya 50 kutoka Jumuiya ya Wazazi, katika kata ya Kolandoto.

Mrindoko amezindua Shina hilo la Wajasiriamali leo, Jumamosi Februari 23, 2024, akiwa katika ziara yake akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini. 

Ziara hiyo imehusisha kutembelea kata za Chamaguha, Ibadakuli, na Kolandoto kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na uhai wa chama.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mrindoko amesema kuwa ufunguzi wa shina hilo utawezesha wajasiriamali hao kupata mikopo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, na hivyo kujiinua kiuchumi.

Kupokea Wanachama Wapya

Mrindoko amewapongeza wanachama wapya walioungana na Jumuiya ya Wazazi CCM katika kata ya Kolandoto na kusisitiza kuwa uhai wa CCM unategemea idadi kubwa ya wanachama, hasa wanaolipa ada za uanachama.

Wanachama wapya wa Jumuiya ya Wazazi CCM kata ya Kolandoto wakionesha kadi zao

Ukaguzi wa Miradi ya Ujenzi

Akiwa katika kata ya Ibadakuli, Mrindoko, pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji, wametembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa matundu ya vyoo na mabweni katika Shule ya Sekondari Rajani.

 Amewataka wakandarasi wa miradi hiyo wahakikishe wanakamilisha kazi zao kwa wakati, akisema  tarehe ya mwisho ya Machi 10 ,2025 aliyoahidi kukamilisha kazi iwe ya kweli.

Wito wa Wazazi na Walezi

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji, Daniel Kapaya, amewahimiza wazazi na walezi kuchukua hatua madhubuti kulinda watoto wao na kuhakikisha wanapata lishe bora ili waweze kukua vizuri.

 Amewataka wazazi kutoa chakula cha mchanganyiko kwa watoto shuleni ili kudhibiti utapiamlo.

 Daniel Kapaya 

“Akina mama naomba tunyonyeshe watoto wetu, lakini pia tuwape chakula wanafunzi shuleni. Wazazi mnakula zaidi ya watoto, naomba msiwe wachoyo, msiwapunje watoto chakula, changieni chakula shuleni lakini pia tuhakikishe tunawapa watoto chakula mchanganyiko ili kukabiliana na utapiamlo”,amesema Kapaya.

Afya ya Jamii

Mjumbe mwingine, Boniphace Giti, amehimiza wananchi kufanya mazoezi na kutumia huduma za hospitali na vituo vya afya ili kufanya uchunguzi wa afya zao mapema, badala ya kutegemea waganga wa kienyeji.

Maoni ya Wajumbe

Wajumbe wengine wa Kamati ya Utekelezaji, Zulfa Hassan, Mary Makamba, na Mhandisi James Jumbe, wamesisitiza kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuleta maendeleo kwa wananchi.

 Wamesisitiza kuwa “Wajibu wa Makada wa CCM ni kuyasema mazuri yote anayofanya Rais Samia.”

Usajili wa Wanachama

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Kibabi, amesisitiza umuhimu wa vikao vya kikatiba na kikanuni, pamoja na kuhamasisha usajili wa wanachama wapya ili kuendeleza idadi ya wanachama na kuongeza nguvu ya chama.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko (wa pili kushoto), akizindua Shina la Wakereketwa la Wajasiriamali katika tawi la Chamaguha, kata ya ChamaguhaMwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko akipandisha bendera ya CCM wakati akizindua Shina la Wakereketwa la Wajasiriamali katika tawi la Chamaguha, kata ya Chamaguha

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Kibabi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shina la Wakereketwa la Wajasiriamali katika tawi la Chamaguha, kata ya Chamaguha

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko akizungumza wakati akizindua Shina la Wakereketwa la Wajasiriamali katika tawi la Chamaguha, kata ya Chamaguha

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Chamaguha
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mary Makamba akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Chamaguha
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Boniphace Giti akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Chamaguha
Sehemu ya wanachama na viongozi wa CCM kata ya Chamaguha
Sehemu ya wanachama na viongozi wa CCM kata ya Chamaguha
Diwani wa Kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhan akizungumza wakati wa kikao
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko akizungumza katika kata ya Ibadakuli
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko na wajumbe wa kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa vyoo katika shule ya Sekondari Rajani katika kata ya Ibadakuli
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko na wajumbe wa kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari Rajani katika kata ya Ibadakuli
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko na wajumbe wa kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari Rajani katika kata ya Ibadakuli
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko na wajumbe wa kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari Rajani katika kata ya Ibadakuli
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko akizungumza katika kata ya Ibadakuli
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko akizungumza katika kata ya Ibadakuli
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ibadakuli
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ibadakuli
Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ibadakuli
Diwani wa Kata ya Ibadakuli, Msabila Malale akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ibadakuli
Diwani wa Viti Maalumu Mhe. Zuhura Waziri akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ibadakuli
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Daniel Kapaya akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ibadakuli
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mary Makamba akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ibadakuli
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ibadakuli
Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akikabidhi kadi kwa mmoja wa wanachama wapya wa Jumuiya hiyo kata ya Kolandoto

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko akizungumza katika kata ya Kolandoto
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ndg. Fue Mrindoko akizungumza katika kata ya Kolandoto
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto

Diwani wa kata ya Kolandoto, Mhe. Mussa Elias akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM 
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Boniphace Giti akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Daniel Kapaya akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Zulfa Hassan akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Richard Mseti ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mary Makamba akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kolandoto .
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

About the author

mzalendoeditor