Featured Kitaifa

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO KWA VIONGOZI WANAWAKE WENYEVITI WA MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI MKOANI SIMIYU

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Bariadi – Simiyu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa *Ndg. Mary Chatanda (MCC)* amefungua Mafunzo ya Viongozi Wanasiasa Wanawake Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji Mkoani Simiyu huku akiwataka kufanya kazi Kwa bidii na weledi Kwa kuwatumikia Watanzania.

*Chatanda,* amesema kuna umuhimu wa viongozi Wanawake kupata mafunzo ikiwa ni mwendelezo wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania kutoa mafunzo kwa viongozi na Watendaji ili wapata uelewa wa pamoja kwenye kutekeleza majukumu ya msingi kwa wanawake na Wananchi kwa ujumla.

Chatanda ameyasema hayo leo (Feb 19, 2025), wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea Uwezo wa kutekeleza majukumu yao, yaliyoandaliwa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), katika ukumbi wa Makuti Longue Mjini Bariadi.

Amesema lengo la mafunzo hayo kwa wanawake viongozi wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji ni kupata nyenzo muhimu kwenye kutekeleza majukumu yao na kwamba lengo la UWT ni kuhakikisha kiongozi mwanamke anatekeleza vema majukumu yake na kuwa mfano na kimbilio la Wananchi.

Chatanda alikuwa Mgeni Rasmi katika Mafunzo hayo huku aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Bara *Ndg. Riziki Kingwande (MNEC)* katika Mafunzo ya Viongozi Wanasiasa Wanawake Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji Mkoa wa Simiyu. 

About the author

mzalendo