Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA WAZIRI RIDHIWANI KWA USIMAMIZI WA MIRADI YA NSSF ARUSHA

Written by mzalendoeditor

Na Mwandishi wetu: Arusha
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kuusimamia Uwekezaji wa Miradi inayotekelezwa naMfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mradi wa majengo ya kitega Uchumi na Mafao House.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq amesema miradi hiyo ikiendelea kutunzwa vema itasaidia kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla

Vile vile, Wajumbe wa kamati hiyo wameshauri NSSF kuendelea kuwekeza kwenye miradi yenye tija na ambayo itasaidia kuingiza kipato serikalini.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza uongozi wa Mfuko wa NSSF kwa kutoa huduma bora kwa wanachama wa mfuko huo, pia kwa usimamizi wa miradi iliyobeba fedha za wananchama.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi wa NSSF, Masha Mshomba amesema jengo la kaloleni kwa mwaka wa fedha 2024/25 mfuko ulipanga kukusanya kiasi cha shilingi milioni 431.30 kama kodi kutoka kwa wapangaji ambapo hadi kufikia tarehe 31 Januari, 2025 mfuko ulifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 277 sawa na 64% ya lengo la makusanyo ya mwaka.

Katika upande wa jengo la Mafao House makusanyo na thamani ya jengo katika mwaka wa fedha 2024/2025 mfuko ulipanga kukusanya kiasi cha shilingi million 1,062 kama kodi kutoka kwa wapangaji na hadi kufikia tarehe 31,Januari 2025, mfuko umefanikiwa kukusanya shilinigi milioni 509 sawa na sasilimia 48 ya lengo la makusanyo ya mwaka.

About the author

mzalendoeditor