Featured Kitaifa

KIGOMA YAPATA MWAROBAINI WA UKATILI WA KIJINSIA.

Written by mzalendoeditor

Na WMJJWM,Kigoma.

Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Elisante Mbwilo amewataka Maafisa Maendeleo ya jamii, Maafisa Masoko, Wenyeviti wa Masoko, polisi na Wawakilishi kutoka Shirikisho la Umoja wa Machinga kuhakikisha ukatili katika mazingira ya umma unadhibitiwa kwa kuwachukulia hatua stahiki wale wote wanaojihusisha na ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma.

Mafunzo ya muongozo wa uanzishaji wa madawati ya kupinga ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma hususani sokoni yamefanyika Februari 12,2025 Mkoani Kigoma.

“Tunafahamu kuwa maeneo ya Umma yamehusisha maeneo mengi hususan maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi na maeneo yaliyo wazi kama vituo vya mabasi, masoko, mialo na maeneo ya uvuvi, vituo vya michezo nakadhalika hivyo Nichukue fursa hii kuwasihi mfatilie kwa makini mafunzo haya ili yaweze kuwa na tija kwenu na kwa jamii kwa ujumla ili tuweze kutimiza lengo lililokusudiwa la kuanzishwa kwa Mwongozo huu”.Amesema Mbwilo

Naye Mkurugenzi Msaidizi idara ya Maendeleo ya Jinsia Rennie Gondwe ametoa rai kwa Maafisa Maendeleo ya jamii, Maafisa Ustawi wa jamii Maafisa Masoko, Wenyeviti wa Masoko, polisi na Wawakilishi kutoka Shirikisho la Umoja wa Machinga kutumka Mwongozo huo kama chachu ya kupunguza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwenye maeneo yote ya Umma.

“Maeneo haya yamekuwa na malalamiko mengi ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni pamoja na lugha chafu za udhalilishaji, miundombinu mibovu ya utendaji kazi, kukosekana kwa Usawa wa ushiriki wa Wanawake kwenye nafasi za Uongozi na maamuzi, kutokuwa na mazingira salama ya watoto wanaofika kwenye maeneo hayo pamoja na kukosekana kwa madawati ya Kijinsia yanayoweza kusaidia wahanga wanaofanyiwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia”amesema Rennie.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo wa Mkoa Msafiri Nzunuri amejidhatiti kufanya kazi kwa ukaribu na mamlaka zote husika ili Kudhibiti ukatili wa kijinsia na kuhakikisha manusra wa ukatilo wanapata haki inayostahili katika Mkoa wa Kigoma.

About the author

mzalendoeditor