Featured Kitaifa

RC RUVUMA AIPONGEZA EWURA, KUDHIBITI SEKTA YA MAFUTA KWA WELEDI

Written by mzalendoeditor

 

Meneja wa EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mhandisi. Karim Ally (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed, mara alipo wasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo leo 11.2.2025, Ruvuma.

……..

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali. Ahmed Abbas Ahmed, ameipongeza EWURA, kwa kuwadhibiti wafanyabiashara wajanja waliokua wakitishia kuficha mafuta kwa kisingizio cha kusubiri bei mpya ya mafuta itangazwe.

Ameyasema leo Tar.11.2.2025, wakati alipotembelewa na Meneja wa EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mha. Karim Ally, kwa lengo la kuzungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi hiyo ya kanda.

“Hongereni sana EWURA, kuweza kuwadhibiti wafanya biashara wa mafuta wasio waaminifu. Huduma zimekua nzuri wakati wote, pia nawapongeza kwa huu mfumo wenu wa NPGIS, ambao unawasaidia kujua kiasi cha mafuta kilichopo katika vituo vya mafuta” alisema

Pia Kanali Ahmed alitoa rai kwa EWURA kutoa elimu zaidi ya matumizi ya gesi ya kupikia majumbani na gesi asilia kwenye magari ili wananchi wengi wachangamkie fursa hizo mara moja.

Mhandisi Ally alisema ni jukumu la EWURA ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za nishati na maji kwa wakati na kwa gharama sahihi.

Ofisi ya EWURA nyanda za Juu Kusini ina ofisi zake katika jengo la NHIF, Ghorofa ya 6 Mbeya na inasimamia mikoa mitano ukiwepo mkoa wa Ruvuma, Mbeya, Njombe, Songwe na Rukwa

About the author

mzalendoeditor