Featured Kitaifa

MCC CHATANDA ASHIRIKI MAZISHI YA SHEMEJI YAKE MCC RAJABU

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Pangani ~ Tanga.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), *Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC)* ameshiriki Mazishi ya Shemeji yake *Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Ndg. Rajabu Abdullahman Abdullah (MCC)* msiba uliotokea tarehe 09 Februari, 2025, Wilayani Pangani.

*Aidha,* MCC Chatanda alipata nafasi ya kutoa Salamu za Pole na aliwakumbusha kuwa Tarehe 13 Febuari, 2025 litaanza zoezi la uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga hivyo watu wote wenye sifa ya kujiandikisha wajitokeze Kwa wingi kujiandikisha.

Msiba huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama akiwepo *Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Batlida Buriani,* Mbunge wa Bumbuli Mhe. Januari Makamba(MNEC), Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu, Mbunge wa Handeni Vijijini, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Gift Musuya, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Zainabu Abdallah na Wengine wengi.

About the author

mzalendo