Featured Kitaifa

MAJALIWA MGENI RASMI KILELE CHA WIKI YA ANWANI ZA MAKAZI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 08, 2025 ni mgeni rasmi katika maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Anwani za Makazi inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC).

Utekelezaji wa oparesheni ya mfumo wa anwani za makazi nchini umewezesha ukusanyaji wa taarifa milioni 12.3 za anwani za makazi ambazo zimehifadhiwa katika mfumo wa kidijitali unaojulikana kwa jina la National Physical Addressing (NaPA).

Mfumo wa anwani za makazi ni daftari la kidijitali la wakazi na makazi kwa ajili ya ambalo linawezesha kuharakisha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii na kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuwezesha biashara mtandao na kufanyika kwa ufanisi pamoja na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na majanga.

kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni *“tambua na tumia anwani za makazi kurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma”.*

About the author

mzalendoeditor