Featured Kitaifa

WASIRA ASEMA CCM ITABEBA CHANGAMOTO IKIWEMO YA BARABARA ZA LAMI MARA

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasira, amewahakikishia wananchi mkoani Mara kuwa Chama kitaendelea kuzibeba changamoto zinazowakabili na kuendelea kuzitafutia ufumbuzi.

Miongoni mwa changamoto hizo ni ujenzi wa baadhi ya barabara ambazo zinapaswa kujengwa kwa lami ili kuzifungua baadhi ya wilaya za mkoa pia kuiunganisha Mara na nchi jirani ya Kenya kwa barabara za lami.

Wasira aliyasema hayo leo Rorya mkoani Mara alipokuwa akizungumza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Rorya.

“Sisi ni Chama Cha Mapinduzi, kazi yetu ni kusikiliza kero za watu, mnaweza tukacheza ngoma, lakini kama matatizo ya watu hayazungumzwi na hayatafutiwi ufumbuzi watu watakuwa hawana hakika kama Chama hiki kinashughulika na matatizo yao.

“Sasa nimemuelewa rafikiangu wa TANROADS tatizo lake la bajeti, anapewa sh. bilioni moja, kwa hiyo kama anatengeneza sana ni kilometa moja au moja na robo, na kwa kuwa barabara ina kilometa 56 maana yake ataikamilisha kwa miaka 56.

Wasira alilazimika kueleza hayo baada ya Mbunge wa Rorya (CCM) Jafari Chege kueleza kuwa miongoni mwa changamoto za jimbo hilo ni baadhi ya barabara kutokuwa za kiwango cha lami.

About the author

mzalendo