Featured Kitaifa

WANANCHI 161,154 WAFIKIWA NA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA GEITA

Written by mzalendoeditor

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) imewafikia wananchi 161,154 katika Mkoa wa Geita ambapo kati yao wanaume ni 80,810 na wanawake ni 80,344.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Kampeni hiyo Mkoa wa Geita Wakili wa Serikali Candid Nasua wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kampeni hiyo kwa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Mohamed Gombati leo Februari 6, 2025.

“Hadi kufikia Februari 04, 2025 tulifanikiwa kukamilisha zoezi la Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya mama Samia ambapo tumefika katika Halmashauri zote za Mkoa na malengo ya Wizara yametimia katika Kata na Vijiji/Mitaa iliyopangwa kufikiwa wakati wa Kampeni hii na tunashukuru sana Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano tuliopewa katika kufanikisha Kampeni hii Muhimu kwa Taifa” Amesema Nasua

Aidha Nasua amesema kuwa jumla ya Migogoro 584 imepokelewa wakati wa Kampeni ambapo Migogoro 86 imetatuliwa papo kwa papo na Migogoro 498 inaendelea kushughulikiwa.

Kwa Upande wake Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Mohamed Gombati amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuifikisha Kampeni hiyo kwa wananchi wa Geita ambapo imekuwa na manufaa makubwa.

Kampeni hiyo pia iliambatana na utolewaji wa huduma ya usajili waw a matukio muhimu ya bundamu iliyotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ambapo jumla ya wananchi 721 wamefikiwa na huduma hiyo, Sambamba na Uchangiaji wa damu salama, Upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza, Uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa kizazi na Uzazi wa Mpango.

About the author

mzalendoeditor