Featured Kitaifa

KATAMBI UNDER 17 CUP 2025 KULETA PAMOJA VIJANA SHINYANGA MJINI

Written by mzalendoeditor
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), bwa. Samwel Jackson (kulia) akikabidhi fedha kwa Wajumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga (SHIDIFA) ikiongozwa na mwenyekiti wake Joseph Assey (wa pili kushoto) kwa ajili ya Mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama Katambi Under 17 Cup 2025

Na Kadama Malunde -Malunde 1 blog

Mashindano ya mpira wa miguu yanayojulikana kama SHIDIFA Under 17 League, maarufu kama Katambi Under 17 Cup 2025, yanatarajiwa kutimua vumbi kuanzia Februari 14, 2025, huku timu 16 zikishiriki kwa udhamini wa kipekee kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Mashindano haya, ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya michezo kwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 17, yanatarajiwa kuwa jukwaa la kuibua vipaji vya vijana wa mtaa na wanafunzi wa shule za sekondari. 

Fedha ya shilingi milioni 4 kati ya shilingi milioni 6,610,000/- alizotangaza kudhamini Mbunge Katambi, tayari leo Februari 5,2025 zimekabidhiwa kwa Wajumbe wa Kamati tendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga (SHIDIFA) ikiongozwa na mwenyekiti wake Joseph Assey ikiwa ni dhamiracya dhati ya Mbunge huyo kusaidia maendeleo ya michezo katika jimbo lake.

Mbunge Katambi, kupitia kwa Katibu wake Samwel Jackson, amesisitiza umuhimu wa michezo kwa vijana kama njia ya kuleta maendeleo na ajira. 

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), bwa. Samwel Jackson (katikati) akizungumza wakati akikabidhi fedha kwa Wajumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga (SHIDIFA) kwa ajili ya Mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama Katambi Under 17 Cup 2025

Ameeleza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha vijana kutoka katika shule na jamii wanapata fursa ya kuonyesha vipaji vyao na pia kujifunza kupitia michezo.

Amesema Mhe. Mbunge anataka kuona vijana hawa wanapata nafasi ya kujiendeleza katika michezo na kuwa na mafanikio ya kimaisha.

“Tulipokea barua kutoka SHIDIFA wakiomba Mhe. Mbunge afadhili mashindano ya chini ya miaka 17, ambapo Mbunge aliridhia kudhamini mashindano haya ya wilaya ya vijana wetu ambayo yanaibua vipaji. Bajeti nzima ya mashindano ilikuwa Shilingi 6,610,000/- na kwa kuwa michezo hii inatakiwa ianze mapema mwezi huu, siku ya leo Februari 5,2025 anakabidhi shilingi Milioni 4 kwa kuanzia ili mashindano yaende na pesa iliyobaki atamalizia wakati mashindano yanaendelea”,amesema Jackson.

“Mhe. Mbunge anapendai sana michezo na  anawatakia wanamichezo, michezo mema na pindi atakaporejea Jimboni atakuja kuwaona kwenye viwanja tofauti ambapo michezo itakuwa inaendelea”,ameeleza  Jackson.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga (SHIDIFA), Joseph Assey, ameeleza furaha yake kutokana na ufadhili wa Mbunge Katambi, akisisitiza kuwa mashindano haya yatasaidia kuongeza mshikamano na ufanisi wa vijana. 

“Mhe. Katambi ameonyesha kujali sana maendeleo ya vijana na michezo, na tunamshukuru kwa kuleta matumaini makubwa kwa jamii ya Shinyanga”,amesema Assey.

“Tunatoa shukrani kubwa kwa Mhe. Katambi. Kuwaweka vijana pamoja ni jambo jema sana, tulikuwa tunalia na wadhamini na sasa tuna furaha kubwa ndani ya mioyo yetu kwa sababu tutaenda kuendesha mashindano haya kwa urahisi, vijana wapate zawadi, wapate jezi, wang’ae vizuri katika mashindano haya yatakayochukua muda wa mwezi mmoja, yakishirikisha baadhi ya shule na timu zingine za mtaani ndani ya Manispaa ya Shinyanga”,amesema Assey.

Katibu Mkuu wa SHIDIFA, Budete Njile, amesema mashindano yatakuwa yakifanyika kila Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, ambapo wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu watashiriki kwa umri wa miaka 15 hadi 17.

Mashindano yatashirikisha timu 16, ikiwa ni pamoja na timu za shule za sekondari binafsi kama Istiqaama na Little Treasures pamoja na shule za serikali kama Masekelo na Mwasele, yatafanyika kwenye viwanja mbalimbali ikiwemo Istiqaama na Sabasaba. 

Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025 ni muhimu kwa wilaya ya Shinyanga, kwani yanatoa fursa kwa vijana wengi kupata mafunzo ya kimaisha kupitia michezo, huku pia wakionyesha vipaji vyao kwa jamii na wadhamini. 

Mashindano haya yatakuwa sehemu muhimu ya kubaini na kukuza vipaji vya vijana, huku pia vijana wakichangia katika kuleta burudani kwa jamii.

Hii ni moja ya mikakati ya Mbunge Katambi ya kuleta maendeleo kwa vijana na michezo katika jimbo lake.

About the author

mzalendoeditor