Featured Kitaifa

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA YAWAFIKIA WANANCHI MPANDA

Written by mzalendoeditor

 

Timu ya Wataalam ya kampeni ya msaada wa kisheria wa mama Samia Legal Aid (MSLAC) ikiongozwa na Salome Mwakalonge ambaye ni Mratibu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria imeendelea kutoa elimu ya kisheria kwa Wananchi wa Manispaa ya mpanda ambapo wamefanikiwa kutatua mgogoro baina ya Wananchi wa kawanzige na Gereza la Kalilankulukulu juu ya kuingiza mifugo na kulisha mazao yaliiyopo kwenye eneo la Gereza kinyume na Sheria.

Mkuu wa Gereza la Kalilankulukulu SSP Joseph Mkalaba amesema walikamata mifugo 29 (ng’ombe) zilizo ingizwa eneo la Gereza na kulisha mazao kinyume na Sheria.

Mkuu huyo ameendelea kwa kusema kuwa wanaishukuru timu ya msaada wa kisheria wa mama Samia kuja kutoa elimu ya kisheria kwa Wananchi wa kawanzige na kufikia makubaliano mazuri na kutatua mgogoro huo na Gereza na kuachilia huru mifugo hiyo.

Kwa upande wao Wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya Gereza wameishukuru timu inayotoa elimu ya masuala ya kisheria kwa kuwapatia elimu na kuweza kutatua mgogoro huo kati yao na Gereza.

Kampeni ya kutoa elimu ya msaada wa kisheria wa mama Samia kupitia timu ya Wataalam imefanikiwa kutoa elimu ya kisheria ya masuala ya ndoa,miradhi,wosia na ukatili Kata ya Mwamkulu mtaa wa mkwajuni,Senso na kabwaga Manispaa ya Mpanda.

About the author

mzalendoeditor