Featured Kitaifa

TAKUKURU DODOMA YAOKOA MIL 66 ZILIZOKUWA HAZIJAPELEKWA BENKI KONDOA

Written by mzalendoeditor
MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw.Victor Swella,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 29,2025 jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha Oktoba- Disemba 2024.
Na Alex Sonna,Dodoma
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kuokoa Shilingi milioni 66 za makusanyo ya POS mashine zilizokuwa hazijapelekwa benki katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa.
Hayo ameelezwa leo Januari  29,2025 Jijini Dodoma na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma,Bw.Victor Swella wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha Oktoba- Disemba 2024 kwa Waandishi wa Habari.
Bw.Swella amesema Takukuru Mkoa wa Dodoma katika kuhakikisha inasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato  katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma ilikuja  na utaratibu wa kupata taarifa za makusanyo ya POS kwa kila Halmashauri Kila Jumatatu.
Amesema lengo ni kubaini kama Kuna makusanyo hayajapelekwa benki  kama utaratibu unavyotaka ili kuchukua hatua mapema ya kudhibiti Hali hiyo kabla ya ubadhirifu mkubwa kufanyika.
Aidha  amesema katika kufuatilia huko waliweza kuokoa Shilingi milioni 66 zikizokuwa hazijapelekwa benki katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa.

About the author

mzalendoeditor