Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
Viongozi wa Halamshauri ya kigoma wameipongeza wizara ya katiba na sheria kwa kuanzisha mafunzo kwa maafisa wa wilaya hiyo kuhusu utawala bora na sheria
Wakizungumza baada ya kupata mafunzo hayo baadhi ya washiri wamesema kuwa ubunifu uliyofanywa na wizara ya katiba na sheria itasaidia kuboresha utendaji kazi mzuri kwa watumishi hao na kufuata misingi ya utumishi bora na sheria.
Bwana Charles Fredy ambaye ni mshiriki wa mafunzo hayo amesema kuwa mada zilizotolewa na wakufunzi wa mafunzo hayo zinasaidia kuwakumbusha wao kama watumishi wa umma kufuata sheria na taratibu za kazi.
Naye Bi.Petronia Bwakila ambaye ni mkuu wa kitendo cha taka na mazingira kutoka kigoma jiji amesema kuwa mafunzo hayo yanawakumbusha kutambua haki na wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao pindi wanapowatumikia wananchi na kuiomba serikali kuongeza muda zaidi wa mafunzo ili kuwajengea ueelewa zaidi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kigoma Mjini Bw.Rashid Chuachua mempongeza waziri na katiba Dkt.Damasi Ndumbaro kwa kutoa mafunzo hayo ngazi za juu na kuwafikia wananchi wa chini.
Amesema kuwa wizara hiyo imefanya jambo la msingi kuwapatia viongozi hao huku akiwataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi kuwa kuzingatia maadili na sheria za kazi.