Featured Kitaifa

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KUTATUA MIGOGORO SEKTA YA MADINI GEITA.

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela amewasihi wananchi wa Mkoa wa huo kujitokeza kutumia fursa ya kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) ili kusikilizwa na kupatiwa msaada huo.

Mhe. Shigela amesema hayo leo Januari 26, wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo kwaniaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.

“Tuna kila sababu za kumshukuru Rais wetu mpendwa kwa kutuletea msaada huu sisi wananchi wake wa Geita niwaombe mjitokeze ili mpate msaada wa migogoro inayowakabili hasa katika sekta ya madini ” Amesema Mhe. Shigela

Nae mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Alfred Dede amewaeleza wananchi hao kuwa baada ya uzinduzi kampeni hiyo itaendelea kwa siku tisa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Geita kuanzia Januari 27, 2025.

About the author

mzalendoeditor