Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ,Bw.Gerson Msigwa, akizungumza na waandishi wa habari Katika stesheni ya Samia Suluhu Dodoma wakati akielekea Mkoani Morogoro ambapo anatarajia kuzungumza na Vyombo vya Habari kesho January 25,2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Gerson Msigwa,akielekea kupanda Treni Katika stesheni ya Samia Suluhu Dodoma wakati akielekea Morogoro ambapo anatarajia kuzungumza na Vyombo vya Habari kesho January 25,2025
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Gerson Msigwa,akiwa ndani ya Treni , akizungumza na wananchi mbalimbali wakati akielekea Mkoani Morogoro ambapo anatarajia kuzungumza na Vyombo vya Habari kesho January 25,2025
Waandishi wa habari kutoka Vyombo mbalimbali wakiwa ndani ya Treni wakielekea Mkoani Morogoro tayari Kwa kazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ,Bw.Gerson Msigwa,ambaye anatarajia kuzungumza na Vyombo vya Habari kesho January 25,2025
Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imesema mpaka sasa abiria milioni 1.5 wamesafiri kwa kutumia treni ya abiria katika kiwango cha kimataifa (SGR) na hivi karibuni itaanza kusafirisha mizigo ambapo tayari imeingiza mabehewa 264 na mengine 264 yapo bandarini na itakuwa na uwezo wa kusafirisha tani 10,000 kwa wakati mmoja.
Kutokana na hali hiyo imewahakikishia watanzania treni zipo za kutosha na mradi unaenda vizuri na wataendelea kufurahia huduma za usafiri.
Hayo yameelezwa leo Januari 24,2025 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Gerson Msigwa,wakati akizungumza na waandishi wa habari Katika stesheni ya Samia Suluhu Dodoma kuelekea Morogoro ambapo anatarajia kuzungumza na Vyombo vya Habari kesho January 25,2025
Bw.Msigwa amesema wanashukuru mradi wa SGR unaendelea kufanya kazi na treni zinazoendelea kufanya kazi kati ya Dodoma na Dar es salaam ambapo matokeo yamekuwa makubwa na zinatoa msaada mkubwa kwa watanzania.
Amesema takwimu mpaka sasa zinaonesha wamesafisha abiria milioni 1.5 ambapo wanasafirisha kwa wastani wa abiria 300,000 kwa mwezi mmoja.
“Treni zinaenda vizuri na zipo za kutosha kwa mahitaji yote.Inawezekana kuna matukio ya kukosa tiketi lakini haina maana kwamba tuna upungufu tunaweza tukaona treni imejaa asubuhi pengine ya mchana ikawa imepungua kidogo ila jioni inakuwa imejaa,”amesema Msigwa
Amesema wameingiza vichwa vya treni 17, mabehewa ya abiria zaidi ya 78 mpaka 80 na mengine yanaendelea kuja.
Msigwa amesema kumekuwa na changamoto za hapa na pale lakini hazihusiani na ubora wa mradi ambapo zinatokana na vitu vidogo vidogo.
Amesema changamoto ya umeme ilitokana na umeme wa gridi ya Taifa ila hawajapata changamoto yoyote kubwa ambazo zinaweza kuwarudisha nyuma.
Pia amesema kwa upande wa kipande cha kwanza kutoka Dare salaam mpaka Morogoro na Dodoma kinaenda vizuri na watanzania wanaendelea kufurahia huduma.
Aidha,Msigwa amesema wanaendelea kukamilisha utaratibu wa kusafirisha mizigo kwani wameingiza mabehewa 264 ya kubeba mizigo na mengine 264 yapo bandarini na muda wowote yatashushwa kuanzia sasa.
“Kazi ya kujenga vipande vingine inaendelea na tunategemea itakapofika Tabora,Mwanza na Kigoma tutakuwa na mizigo mingi inayosafirishwa kwa njia ya reli hii.
“Naomba niwahakikishie watanzania kwamba mradi wao unakwenda vizuri matokeo ni makubwa na watanzania wanafurahia huduma na niwahakikishie Mheshimiwa Rais amedhamiria,”amesema Msigwa.
Msigwa amesema mradi huo utakaogharimu zaidi ya Sh trioni 23 lazima utakamilika kwa wakati.
Amesema mabehewa yanayokuja yatakuwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 10,000 kwa wakati mmoja.