Featured Kitaifa

ZANZIBAR IMETEKELEZA ILANI YA CCM KWA MAFANIKIO MAKUBWA – MHE. ABDULLA

Written by mzalendo
Na MwandishiWetu, Dodoma.
Mjumbe wa kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), taifa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha miaka minne kwa mafanikio ya makubwa ambapo Maagizo na maelekezo ya Ilani hiyo yametekelezwa na mengine yamevuka malengo yaliyopangwa.
Mhe. Abdulla ameyabainisha hayo leo Januari 19,2025 hapa Jijini Dodoma wakatinakitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa kipindi cha miaka minne 2020 – 2024.
Amesema kuwa Serikali hiyo imeboresha mazingira bora kwa wafanyabiashara wa Unguja na Pemba kwa kujenga miradi mikubwa ya masoko na stendi ikiwemo ambapo ameyataja kuwa ni ujenzi wa masoko ya Mwanakwerekwe, Jumbi, Chuini kwa Nyanya pamoja na ujenzi wa vituo zaidi ya 14 kwa wajasiriamali.
“Serikali imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 34 kwa ajili ya kuwapatia mikopo hiyo na hadi sasa Mfuko huo umeshatoa Shilingi Bilioni Thelathini na Moja kwa Unguja na Pemba ambapo Mikopo hiyo imewawezesha wananchi zaidi ya 24,000 na kuzalisha ajira mpya 75,000,”amesema.
Akizungumzia mafanikio ya sekta ya utalii Mhe. Abdulla amesema  mchango wa utalii katika pato la Taifa umefikia asilimia 30 ambapo idadi ya watalii imeongezeka kutoka 260,644 mwaka 2020 hadi kufikia 736,755 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 183. 
“Mafanikio haya yamechangiwa kutokana na kazi ya Uandaaji wa Filamu na Makala ya Kuutangaza Utalii (The Tanzania Royal Tour) ambayo uliiongoza wewe Mhe. Rais na kuvitangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania Bara na Zanzibar Pamoja na uboreshaji wa miundombinu, mawasiliano na uwekezaji wa hoteli za kisasa ambapo miradi ya maendeleo ya utalii imeongezeka kutoka 995 mpaka 1,695,”amesema.
Aidha ameongeza kuwa  huduma ya Umeme inaendelea kusambazwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba, Serikali ikiwa imepeleka huduma ya umeme katika vijiji 222 (Unguja 139 na Pemba 83) sawa na zaidi ya asilimia 72.
Amesema gharama za uunganishaji wa huduma ya umeme zimepungua kutoka Shilingi Laki Nne na Sitini na Nne (464,000) hadi Shilingi Laki Mbili (200,000) kwa wateja wasiozidi urefu wa mita 30 na kwa mteja wa nguzo moja ni kutoka Shilingi Milioni 8 Moja na Laki Saba (1,700,000/-) hadi 200,000/- (kwa maelezo zaidi rejea ukurasa wa 24 na 25).

About the author

mzalendo