Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA UAPISHO WA RAIS WA MSUMBIJI

Written by mzalendoeditor
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo baada ya Rais huyo kuapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Maputo, Januari 15, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa  zamani wa Msumbiji, Joaquim Chissano katika sherehe za kumwapisha Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Daniel  Chapo zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Maputo, Januari 15, 2025. Waziri Mkuu alimwakilisaha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye  uapisho huo.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjane wa Rais wa kwanza wa Msumbiji, Mama Graca Machel katika sherehe za kumwapisha Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Daniel  Chapo zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Maputo, Januari 15, 2025. Waziri Mkuu alimwakilisaha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho huo.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Daniel Chapo akizungumza baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo kwenye uwanja wa Uhuru, Maputo, Januari 15, 2025. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo akiapa kuwa Rais wa Nchi hiyo kwenye Uwanja wa Uhuru,  Maputo, Januari 15, 2025.  Kushoto ni  Rais wa Baraza la Katiba , Profesa Duotora  Lucia da Luz Ribeiro. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine  wakishuhudia matukio  mbalimbali katika sherehe za kumwapisha Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Maputo, Januari 15, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo baada ya Rais huyo kuapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Maputo, Januari 15, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa zamani wa Msumbiji, Filipe Nyusi katika sherehe za  kumwapisha Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Maputo, Januari 15, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………..

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 15, 2025 ameshiriki sherehe za uapisho wa Rais wa Msumbiji akimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Maputo,  ambapo baada ya kiapo hicho  Rais Daniel Chapo ametaja vipaumbele vyake ikiwa ni pamoja na kupambana na rushwa, kuimarisha usalama, kuboresha SEKTA za elimu, afya na kilimo. 

Mbali na hayo RAIS, pia Rais Chapo amewaomba wana Msumbiji wafanye kazi kwa ushirikiano pia ameahidi kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali kwa kupunguza  ukubwa wa Baraza la Mawaziri. 

Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio Mondlane kutoka chama cha Podemos aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu uliofanyika  Oktoba 9, 2024. 

Chapo anakuwa Rais wa tano wa Msumbiji, akichukua nafasi ya Filipe Nyusi baada ya kukamilisha mihula miwili ya utawala wake.

About the author

mzalendoeditor