Walezi wa mtoto wa Paulina Nanyoro katika kata ya Hazina Jijini Dodoma wameingia katika sintofahamu ya kupotea kwa mtoto wao wa kike mwenye umri wa miaka 12 kutojulikana alipo kwa kipindi cha muda wa wiki mbili huku wakihofia huenda mtoto huyo ametoroshwa licha ya taarifa hizo kuwa mezani kwa jeshi lapolisi.
Akizungumzia mazingira ya mtoto huyo kupotea majira ya saa 10 jioni mlezi wa mtoto Esupat Saringe amesema alimtuma kitu chumbani nae akiwa chumba kingine na baadae kuhisi mlango wa mtoto huyo ukifunguliwa alipotoka kwenda kumuangalia hakumkuta.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Hazina Azizi Omary amekiri kupokea taarifa ya kupotea kwa mtoto huyo.