Mtandao huo maarufu wa kijamii unaochapisha video fupi umeagizwa pia kufungua ofisi zake nchini Venezuela. Kwa mujibu wa mahakama ya nchi hiyo ni kwamba fedha hizo zitatumika “kuunda hazina ya waathiriwa wa mtandao wa TikTok.”
Mnamo Novemba, Rais wa Venezuela Nicolas Maduro alitishia kuchukuwa “hatua kali” dhidi ya mtandao wa TikTok ikiwa usingeliondowa maudhui yanayohusiana na kile alichokiita “mashindano ya uhalifu.”
Umaarufu wa kimataifa wa mtandao huo wa Kichina unatokana na mashindano yake kama hayo. Lakini mtandao huo umekabiliwa na shutuma kwa kuwaweka watumiaji hatarini kwa kuruhusu kuenea kwa video hatari za mashindano.
Imeandikwa na Idhaa ya Kiswahili ya DW.