Featured Kitaifa

RAIS SAMIA APONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI KILIMANJARO

Written by mzalendo

Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ummy Nderiananga ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Pia amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bwa. Nurdin Babu kwa utendaji mzuri wakusimamia vizuri miradi ya maendeleo.

Mhe. Nderiananga ametoa pongezi hizo leo tarehe 17 Desemba, 2024 katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa huo (RCC) ambacho kimefanyika Ukumbi wa Ofisi ya Mkoa.

About the author

mzalendo