Featured

EWURA YAWATAKA WADAU WA MAFUTA NCHINI KUWEKEZA KATIKA MAENEO YA VIJIJINI

Written by mzalendoeditor
MENEJA  EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher,akizungumza  wakati wa mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani  Kasulu Mkoani Kigoma yenye lengo la kuwejengea uwezo wa masuala ya kiudhibiti wadau wa sekta ndogo ya petroli kutoka mkoa wa Kigoma ukijumuisha washiriki kutoka wilaya zote sita za Kigoma, Kasulu, Kibondo, Kakonko, Buhigwe na Uvinza yaliyofanyika leo Disemba 10,2024.
Na.Mwandishi WetAu-KIGOMA
MENEJA  EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher amewataka wadau wa masuala ya uuzaji wa mafuta kutumia fursa ya kuwekeza katika maeneo ya vijijini ambako kuna uhaba mkubwa wa vituo vya mafuta.
Mhandisi Christopher ametoa wito huo wakati wa mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani  Kasulu – Kigoma jana Disemba 10,2024 yenye lengo la kuwejengea uwezo wa masuala ya kiudhibiti wadau wa sekta ndogo ya petroli kutoka mkoa wa Kigoma ukijumuisha washiriki kutoka wilaya zote sita za Kigoma, Kasulu, Kibondo, Kakonko, Buhigwe na Uvinza.
Mhandisi Christopher amewakumbusha wadau hao  kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma kwa jamii zenye ubora zaidi,kwa kufuata sheria na utaratibu, kwa ufanisi zaidi na pia kwa kutenda haki hivyo kuboresha maisha ya wananchi wote kwa ujumla.
“Nichukue nafasi hii kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu EWURA, kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwahudumia watanzania kwa kuhakikisha wanapata huduma bora za mafuta ya petroli na gesi ya kupikia kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, ” amesema Mhandisi Christopher
Amesema,EWURA, katika kutekeleza majukumu na kazi zake kwenye sekta ndogo ya petroli, inawajibika kuzingatia Sheria ya EWURA Sura ya 414 na Sheria ya Petroli, Sura ya 392 na kufafanua kuwa Chini ya Sheria hizo Mamlaka ina jukumu la kudhibiti kiufundi na kiuchumi mkondo wa kati na wa chini wa sekta ndogo ya petroli kwa Tanzania Bara.
“Lengo letu kuu la udhibiti ni kulinda maslahi ya walaji, wauzaji bidhaa za mafuta na serikali, ambao kwa pamoja ni wadau wakuu wa EWURA, ” amesisistiza
Mbali na hayo ameeleza kuwa kazi za udhibiti zinazotekelezwa na Mamlaka katika sekta hiyo zinalenga kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa za petroli nchini,kuweka gharama stahiki katika ununuzi, uhifadhi, usafirishaji na usambazaji wa bidhaa za petroli na kuvutia uwekezaji ili kusaidia uhakika wa huduma na usambazaji wa bidhaa za petroli nchini kote.
“Malengo mengine ni kuweka mazingira sawia ya kibiashara ili kulinda maslahi ya watoa huduma au wasambazaji wa bidhaa za petroli; na,kutekeleza sera za serikali kama ilivyoainishwa katika Sera ya Nishati, ” ameeleza.
Akizungumzia ushiriki wa wadau hao ameeleza, “kama tunavyojua EWURA katika kutimiza wajibu wake  huwashirikisha wadau muhimu kwenye sekta ya ndogo ya petroli ambao kwa namna moja ama nyingine hushiriki kwa kiasi kikubwa kwenye mnyororo wa biashara ya bidhaa za mafuta ya petroli na gesi ya kupikia, ” amesema na kuongeza;
Hivyo tumewashirikisha pia kwenye semina hii ikiwemo, Wakala wa Vipimo (WMA), Shirika wa Viwango Tanzania (TBS), Baraza za Mazingira za Taifa (NEMC), Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Mamlaka ya Bima ya Taifa (TIRA), Jeshi la Zimamoto, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Halmashauri zetu na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa bidhaa zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC),”amefafanua.
Mhandisi Christopher ameeleza kuwa Sheria ya Petroli, Sura ya 392, vinaipa uwezo Mamlaka kutekeleza majukumu ya udhibiti wa kiufundi na kiuchumi wa sekta ya petroli kupitia utoaji wa leseni ili kusimamia ubora, usalama na ufanisi wa huduma na kwamba  Sheria hiyo, inataka mtu yeyote mwenye nia ya kufanya biashara ya mafuta petroli na gesi ya kupikia, atalazimika kuomba leseni EWURA.
 Sambamba na sheria hizo tajwa,amesema EWURA pia imetunga kanuni na miongozo mbalimbali na kuanzisha mifumo mbalimbali kurahisisha utendaji kazi na kusimamia sekta ndogo ya petroli.
“Semina hii itatupa fursa ya kuwajengea uwezo kujua na kukumbushana sheria na kanuni hizo, miongozo na mifumo iliyopo,hivyo katika mada zilizopo tunajifunza utekelezaji wa majukumu na Wajibu wa EWURA, Sheria na Kanuni za Mafuta ya petroli na Gesi ya Kupikia,ukaguzi wa bidhaa za mafuta ya petroli na mifumo ya kutuma taarifa na namna ya kufanya maombi ya Leseni kwenye mfumo wa maombi ya leseni (LOIS), “amesema
Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wadau hao fursa zilizopo kwenye sekta ndogo ya petroli hususani maeneo ya vijijini ambapo ameeleza kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa vituo vya mafuta na kutolea Mfano kuwa Mkoani Kigoma kuna jumla ya vituo vya mafuta 63 ambapo vituo 53 vipo mijini na vituo kumi (10) tu vipo maeneo ya vijijini.
“Napenda kutoa rai kwenu kuendelea kuwekeza ujenzi wa vituo vya mafuta katika maeneo ya vijijini,fursa nyingine ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao unatoa mwelekeo wa nchi wa kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo mkakati huu una lengo la kuhakikisha kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034,”amesema.
Kutokana na hali hiyo Meneja huyo amewashauri wadau wa mafuta kuwekeza kwenye eneo yenye uhaba kutokana na kupewa msukumo mkubwa na serikali hasa ikizingatiwa kuwa imekuwa ni agenda mahususi ambayo imechukua nafasi kubwa katika Sera, Mipango na Mikakati ya Serikali.
“EWURA inawasihi kuleta maombi kwa wingi ya kuomba leseni ya usambazaji ya gesi ya kupikia ili nishati hii iwafikie watanzania kwa wingi kwa nia ya kuitumia na hivyo kuchangia utunzaji wa mazingira, kuboresha afya, ustawi wa jamii na kukuza uchumi wetu. Kwa sasa Mkoa wa Kigoma una jumla ya wasambazaji wa gesi ya kupikia (LPG) wawili tu, “amesisistiza.
Kwa kudhihirisha hayo amesema EWURA itaendelea kuhakikisha inadhibiti sekta ya mafuta kwa haki, ili huduma hiyo iendelee kupatikana wakati wote na kwa bei stahiki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wauzaji wa mafuta Wilaya ya Kigoma Bw. Salum Ally ameipongeza EWURA kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu kwa wadau wa mafuta nakusema kwamba zoezi hili liwe endelevu na kuziomba taasisi nyingine ikiwemo WMA, TRA NEMC, PPRA, TIRA pamoja na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuiga mfano huo huku baadhi ya wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakiishukuru EWURA kwa hatua hiyo.
Pamoja na Mambo mengine,semina hiyo imefanyika kutokana na utaratibu wa EWURA hufanya mafunzo kama hayo mara kwa mara kwa wadau wa sekta ndogo ya petroli ikiwahusisha wafanyabiashara wa mafuta  ya petroli na gesi ya kupikia nchini ili kuwapatia wafanya biashara hao, elimu kuhusu kazi na wajibu wa EWURA, fursa zipatikanazo katika sekta ya petroli , nyenzo za udhibiti wa biashara ya mafuta na gesi na kuimarisha uelewa wa matumizi ya mifumo mbalimbali ya kurahisisha huduma zitalewazo na  EWURA ambayo ni Mfumo wa Leseni (LOIS) na Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Petroli na Gesi (NPGIS).
Pia semina kama hizo hutoa fursa kuongeza uelewa wa mabadiliko mapya ya kisheria na kanuni katika kuimarisha  shughuli za biashara ya mafuta ya petroli na gesi ya kupikia na naona bora ya kuwahudumia wateja na ushirikiano wakati wa kutekeleza majukumu yetu.
MENEJA Meneja EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher,akizungumza  wakati wa mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani  Kasulu Mkoani Kigoma yenye lengo la kuwejengea uwezo wa masuala ya kiudhibiti wadau wa sekta ndogo ya petroli kutoka mkoa wa Kigoma ukijumuisha washiriki kutoka wilaya zote sita za Kigoma, Kasulu, Kibondo, Kakonko, Buhigwe na Uvinza yaliyofanyika leo Disemba 10,2024.
MWENYEKITI  wa wauzaji wa Mafuta wilaya ya Kigoma Bw.Salum Ally ,akizungumza  wakati wa mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani  Kasulu Mkoani Kigoma yenye lengo la kuwejengea uwezo wa masuala ya kiudhibiti wadau wa sekta ndogo ya petroli kutoka mkoa wa Kigoma ukijumuisha washiriki kutoka wilaya zote sita za Kigoma, Kasulu, Kibondo, Kakonko, Buhigwe na Uvinza yaliyofanyika leo Disemba 10,2024.
MENEJA Meneja EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani  Kasulu Mkoani Kigoma yenye lengo la kuwejengea uwezo wa masuala ya kiudhibiti wadau wa sekta ndogo ya petroli kutoka mkoa wa Kigoma ukijumuisha washiriki kutoka wilaya zote sita za Kigoma, Kasulu, Kibondo, Kakonko, Buhigwe na Uvinza yaliyofanyika leo Disemba 10,2024.
MENEJA Meneja EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani  Kasulu Mkoani Kigoma yenye lengo la kuwejengea uwezo wa masuala ya kiudhibiti wadau wa sekta ndogo ya petroli kutoka mkoa wa Kigoma ukijumuisha washiriki kutoka wilaya zote sita za Kigoma, Kasulu, Kibondo, Kakonko, Buhigwe na Uvinza yaliyofanyika leo Disemba 10,2024.

About the author

mzalendoeditor