Featured Kitaifa

WAHITIMU 9000 WATUNUKIWA SHAHADA NA STASHAHADA CHUO KIKUU UDOM

Written by mzalendoeditor
 
Na.Alex Sonna-DODOMA
MKUU wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena  Tax,amewatunuku jumla ya wahitimu  9,000  wa chuo hicho katika Mahafali ya 15 mwaka huu.
Akitoa hotuba yake chuoni  hapo leo Disemba 6,2024 jijini Dodoma Makamu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Prof. Lughano Kusiluka,amesema hivi sasa UDOM imeanza kuvutia wananfunzi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Pakistan ambapo kuna mwanafunzi mmoja.
“‘Naomba niwatoe hofu kuwa elimu tunayotoa UDOM ni ya viwango,wanafunzi wanaohitimu wamepikwa na kuwa vizuri.Nawapongeza wakufunzi ambao mmekuwa mkisimamia misingi bora ya elimu kwa wanafunzi kuhakikisha wanamaliza wakiwa na nidhamu,” amesema Prof. Kusiluka.
Aidha amesema kuwa Chuo hicho kinatarajia kujenga Hoteli ya nyota tano pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali  ikiwamo ya kiutafiti ambapo kwa sasa kina miradi 72.
Aidha,  Prof. Kusiluka ,amewataka Wahitimu hao wasichague kazi za kufanya kwa kuwa tayari wameshapata maarifa mbalimbali kupitia chuo hicho.
Naye  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Prof. Rwekaza Mukandala,amesema kuwa chuo kinaendelea kusimamia mikakati mbalimbali ya kiufanisi  na kwamba Baraza hilo linaendelea kusimamia utekelezaji wa mpango mkakati wa chuo wa miradi iliyopo.
Prof. Mukandala ametoa shukrani zake za dhati kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeIea kukiunga mkono chuo hicho.
Aidha Prof Mukandala,amewapongeza Wahitimu wote kwa kumaliza masomo yao huku akiwataka kuwatumikia  wananchi na Taifa kwa ujumla.

About the author

mzalendoeditor