Featured Kitaifa

TANZANIA ,AFRIKA KUSINI KUIMARISHA UHUSIANO KATIKA NYANJA ZA SAYANSI,TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Afrika Kusini Mhe. Dkt. Blade Nzimande ambapo wamejadili namna ya kuimarisha uhusiano katika nyanja za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

Waziri Mkenda amemueleza kuwa Tanzania inajivunia uhusiano mzuri na wa kihistoria na Afrika Kusini katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo Elimu, na kwamba ni muhimu nchi hizo kushirikiana katika nyanja hizo ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Nae Dkt. Bonginkosi Nzimande ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua mbalimbali katika kuongeza hamasa ya matumizi ya Sayansi na teknolojia hasa katika dunia ya sasa inayobadilika kwa kasi.

Waziri huyo amesema kuwa Wizara hizo zinakubliana kuendelea kushirikiana kufanya uwekezaji madhubuti katika Saynsi Teknolojia na Ubunifu ili kufikia Nchi ziweze kufikia malengo maendeleo.

Awali akizungumza Mkurugenzi Idara ya Sayansi na Teknolojia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Ladislaus Mnyone amesema ziara ya ujumbe huo inalenga kuchochea juhudi mbalimbali za kuongeza ukuaji wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ili kuboresha maisha ya Watanzania.

About the author

mzalendoeditor