Featured Kitaifa

DKT.MPANGO ATEMBELEA BANDA LA EWURA MKUTANO WA ARGeo-C10

Written by mzalendoeditor

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Umeme kutoka EWURA, Mhandisi Aurea Bigirwamungu (kushoto) akimueleza kuhusu shughuli za EWURA, wakati wa Maonesho ya Kongamano la 10 la Jotoardhi, linaloendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, leo tarehe 23/10/2024.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (kulia) akizungumza jambo alipotembelea banda la EWURA katika Kongamano la 10 la Jotoardhi Afrika linaloendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, leo tarehe 23/10/2024.
Wanaomsikiliza (kutoka kushoto) ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi, Bi. Tobietha Makafu, Kaimu Mkurugenzi wa Umeme, Mhandisi Aurea Bigirwamungu na ofisa Uhusiano Bi. Janeth Mesomapya.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la EWURA katika Kongamano la 10 la Jotoardhi, linaloendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, leo tarehe 23/10/2024, Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa EWURA, Bi. Janeth Mesomapya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdor Mpango (waliokaa,) katika picha ya pamoja na baadhi ya wadhamini wa Kongamano la 10 la Jotoardhi Afrika (ARGEO – C10) wakiwemo EWURA, wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano hilo leo tarehe 23/10/2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

About the author

mzalendoeditor