Featured Kitaifa

MAJIMBO KUMI  MKOA WA DODOMA KUSAMBAZIWA UMEME

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, akiongea na Wanahabari leo tarehe 18 Oktoba, 2024 wakati wa hafla ya kumtambulisha mkandarasi, kampuni ya DERM Group (T) Ltd katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa mkoa, Jijini Dodoma.

…..

🟢✳️Uwekezaji huo utaigharimu Serikali shilingi bilioni 18 katika kipindi cha miaka miwili

🟢✳️Kaya 4,950 zitanufaika na Mradi huo

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, leo tarehe 18 Oktoba, 2024 amempokea rasmi, mkandarasi, kampuni ya DERM Group (T) Ltd; kampuni ya ndani, iliyoshinda kandarasi ya Mradi wa Kusambaza Umeme kwenye vitongoji 150 vya majimbo kumi (10) ya mkoa wa Dodoma; Mradi unaotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka miwili, kuanzia sasa.

Katika hafla hiyo; Mhe. Rosemary Senyamule amemshukuru, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi bilioni 18.2 kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Kusambaza Umeme kwenye Vitongoji (HAMLET PROJECT II) katika vitongoji 150 vya mkoa wa Dodoma ambapo Wateja wa awali wanaotajiwa kuunganishwa na huduma ya umeme, watakuwa 4,950.

“Mkoa wa Dodoma una jumla ya vijiji 580 ambapo kati ya hivyo vijiji 560 vimepata huduma ya umeme kupitia Miradi ya awali ikiwemo REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, REA Awamu ya Pili na REA Awamu ya Kwanza. Aidha, kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili vijiji 20 viko katika hatua mbalimbali za kukamilishwa kwake (Vijiji 17 vya wilaya ya Mpwapwa na vijiji 3 vya wilaya ya Kondoa)”. Amekaririwa Mhe. Senyamule.

Viongozi wa REA; wakiongozwa na Msimamizi wa Miradi Kanda ya Kati, Mhandisi, Aneth Malingumu amemwambia Mkuu wa mkoa wa Dodoma kuwa, vitongoji 1,631 kati ya vitongoji 2,892 sawa na asilimia 56 vimekwisha kupatiwa umeme kupitia Miradi mbalimbali ya Wakala (REA) na TANESCO. Sambamba na hivyo, vitongoji 150 vitapatiwa umeme kupitia Mradi wa vitongoji vya majimbo kwenye mwaka huu wa fedha Fedha wa 2024/25. Aidha, vitongoji 1,111 vilivyosalia vitaendelea kupatiwa umeme kwa awamu nyingine na kulingana na upatikanaji wa fedha.

“Kwa sasa Wakala wa Nishati Vijijini unatekeleza jumla ya Miradi Mitatu (3) katika maeneo tofauti ya mkoa wa Dodoma yenye jumla ya shilingi bilioni 96.8. Gharama hii inajumuisha shilingi bilioni 18.22 za mkataba baina ya mkandarasi, kampuni ya DERM Group (T) Ltd uliosainiwa hivi karibuni, na mkandarasi wake tunamtambulisha leo kwako”.

“Mradi huu, unalenga kufikia vitongoji 150 vya mkoa wa Dodoma ambapo kila jimbo katika majimbo kumi (10) limepata jumla ya vitongoji 15. Kipaumbele cha mradi huu katika maeneo yatakayofikiwa ni huduma za kijamii yakiwemo mashule, hospitali, ofisi za serikali za mitaa pamoja na nyumba za ibada. Vilevile mradi huu utanufaisha kaya 4,950 na utatekelezwa kwa muda wa miezi 24.” Amesema, Mhandisi, Aneth Malingumu.

Majimbo hayo ni pamoja na Chamwino; Mvumi; Kongwa; Chemba; Kondoa Vijijini; Kondoa Mjini; Mpwapwa; Kibakwe; Bahi na Dodoma Mjini.

Naye, Mhandisi, Hadija Mukiza; Msimamizi wa Mradi huo kwa mkoa wa Dodoma amesema kampuni yao [DERM Group (T) Ltd] imejipanga ili kukamilisha Mradi wa kusambaza umeme kwenye vitongoji 150 vya mkoa wa Dodoma kwa haraka na wanataraji kumaliza kabla ya muda wa mkataba kuisha.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, akiongea na Wanahabari, leo tarehe 18 Oktoba, 2024 wakati wa kumtambulisha mkandarasi, kampuni ya DERM Group (T) Ltd; kampuni iliyoshinda kandarasi ya Mradi wa Kusambaza Umeme kwenye vitongoji 150 vya majimbo kumi (10) ya mkoa wa Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa mkoa, Jijini Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, akiongea na Wanahabari leo tarehe 18 Oktoba, 2024 wakati wa hafla ya kumtambulisha mkandarasi, kampuni ya DERM Group (T) Ltd katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa mkoa, Jijini Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, akiongea na Wanahabari leo tarehe 18 Oktoba, 2024 katika hafla hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa mkoa, Jijini Dodoma.

 

Msimamizi wa Miradi Kanda ya Kati, Mhandisi, Aneth Malingumu akitoa taarifa ya Mradi wa Kusambaza Umeme kwenye Vitongoji vya mkoa wa Dodoma pamoja na Miradi mengine inayotekelezwa na Wakala (REA) leo tarehe 18 Oktoba, 2024 wakati wa kumtambulisha mkandarasi, kampuni ya DERM Group (T) Ltd katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa mkoa, Jijini Dodoma.

Msimamizi wa Miradi Kanda ya Kati, Mhandisi, Aneth Malingumu sambamba na Mhasibu Mwandamizi, Bwana Abuu Kwariko kutoka REA wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa hafla hiyo.

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dodoma wakati wa tukio hilo.

About the author

mzalendoeditor