Featured Kitaifa

WAZIRI JAFO AJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA KITONGOJI CHA KIMANI KISARAWE

Written by mzalendoeditor

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kimani wilaya ya Kisarawe  Mkoani Pwani leo Oktoba 12,2024.

Na.Alex Sonna-KISARAWE

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kimani wilaya ya Kisarawe  Mkoani Pwani.

Akizungumza leo Oktoba 12,2024 mara baada ya kujiandikisha Mhe.Dk.Jafo amewahimiza wananchi wa Kisarawe kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika vituo vya kujiandikisha wapiga kura ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Dk.Jafo amesema zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ni muhimu kwa kuwa ni wajibu kushiriki katika kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia wananchi. 

“Viongozi wa serikali za mitaa ndiyo wanaoishi jirani zaidi na wananchi hivyo ni muhimu kushiriki katika kuwachagua wale watakaolinda maslahi ya jamii husika.”amesema Dk.Jafo

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kimani wilaya ya Kisarawe  Mkoani Pwani leo Oktoba 12,2024.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akijiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kimani wilaya ya Kisarawe  Mkoani Pwani leo Oktoba 12,2024.

About the author

mzalendoeditor