Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akifungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo Timu hiyo iliyoongozwa na Bw. Harris Charalambos Tsangarides (hayupo pichani), imewasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Na. Peter Haule na Saidina Msangi, WF, Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amelishukuru Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa kupitia misaada na mikopo nafuu inayoipatia Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Dkt. Nchemba alitoa shukrani hizo Jijini Dodoma, wakati akifungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), iliyowasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na Awamu ya kwanza ya Programu ya Resilient and Sustainable Fund (RSF) ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kuwa Tanzania inatekeleza Program ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Programu hiyo ya Resilient and Sustainable Fund (RSF) baada ya kukidhi vigezo kufuatia uongozi bora wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa masuala ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
‘‘Baada ya kutekeleza kwa mafanikio programu nyingine zilizopita ikiwepo ile ya Dirisha la Dharura ambapo tulipata fedha za kukabiliana na athari za UVIKO-19 (Rapid Credit Facility- (RCF)), na huu wa ECF unalolenga kufufua na kuimarisha uchumi, Tanzania imetimiza sifa ya kutekeleza program ya RSF ambapo tutapata fedha za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kutoka IMF,’’ alisema Dkt. Nchemba.
Alifafanua kuwa Timu za Wataalam wa pande hizo mbili zitakutana na kujadiliana zaidi kuhusu utekelezaji wa Program hizo na masuala yatakayokubalika wakati wa tathimini yatawasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya IMF kwa ajili ya uidhinishwaji na kupata fedha.
Kwa upande wake Kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Charalambos Tsangarides, alisema kuwa Shirika hilo limeridhishwa na utekelezaji wa programu ya ECF ambayo utekelezaji wake utakamilika katika mwaka wa fedha 2025/2026 na kuipongeza Tanzania kwa kupata idhini ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo kutekeleza program ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Alisema kuwa Shirika lilo limeridhishwa na maendeleo mazuri kuhusu vigezo vya utendaji kazi wa programu ya ECF ambapo litapitia taarifa ya utekelezaji wake wakati wa tathmini.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Harris Charalambos Tsangarides, mara baada ya kufungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo Timu hiyo imewasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akifungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo Timu hiyo iliyoongozwa na Bw. Harris Charalambos Tsangarides (hayupo pichani), imewasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Hafla ya ufunguzi wa vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo Timu ya IMF, imewasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF, Bw. Harris Charalambos Tsangarides (kulia), akizungumza jambo wakati Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), alipofungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika hilo, katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo Timu hiyo imewasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) uliofanywa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo Timu ya IMF imewasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Baadhi ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF, wakimsikiliza Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati akifungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo Timu hiyo imewasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa sita kulia), na Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF, Bw. Harris Charalambos Tsangarides (katikati), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali na Timu ya Wataalam kutoka IMF, baada ya hafla ya ufunguzi wa vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo Timu hiyo imewasili nchini kufanya Tathimini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)