MBUNGE wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde,akabidhi mitungi ya gesi kwa taasisi za umma ikiwemo shule za msingi na Sekondari, Vituo vya afya , Zahanati pamoja na Mama Lishe na Baba lishe ili kupunguza adha ya uchafunzi wa mazingira leo Septemba 20,2024 jijini Dodoma
MBUNGE wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde,akabidhi mitungi ya gesi kwa taasisi za umma ikiwemo shule za msingi na Sekondari, Vituo vya afya , Zahanati pamoja na Mama Lishe na Baba lishe ili kupunguza adha ya uchafunzi wa mazingira leo Septemba 20,2024 jijini Dodoma
Na.Alex Sonna-DODOMA
MBUNGE wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde,amekabidhi mitungi zaidi ya 1000 kwa taasisi za umma ikiwemo shule za msingi na Sekondari, Vituo vya afya , Zahanati pamoja na Mama Lishe na Baba lishe ili kupunguza adha ya uchafunzi wa mazingira.
Akizungumza leo Septemba 20,2024 jijini Dodoma mara baada ya kukabidhi Mhe.Mavunde amesema kuwa lengo la kugawa mitungi hiyo ni katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia
” Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kutumia gesi na nishati mbadala na kuacha kutumia mkaa na kuni ili kuepukana na uharibifu wa mazingira nchini na anamini mitungi hiyo itaendelea kulinda mazingira.”amesema Mhe.Mavunde
Hata hivyo amesema kuwa ataendelea kumuunga mkono Rais Samia katika matumizi ya nishati safi Mimi kama Mbunge wenu nitaendelea kupiga hodi katika maeneo mbalimbali ili lengo la asilimia 80 kutumia nishati hiyo liweze kufikiwa.
Aidha Mhe.Mavunde amesema kuwa ataendelea kutoa mitungi ya gesi kwa makundi mbalimbali ya wananchi katika jimbo hilo kwani serikali imedhamiria kumtua mama kuni kichwani.
Katika hatua nyingine amesema serikali imeendelea kuleta maendeleo mbalimbali katika sekta ya barabara, maji, elimu, afya na sekta zingine na kwamba inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule, amempongeza Mhe.Mavunde kwa jitihada mbalimbali anazofanya katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Dodoma huku akieleza kuwa mitungi hiyo ni sehemu ya utunzaji mazingira kwa kutumia nishati mbadala ili kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa lakini pia kupunguza muda wa kupika.
“Asante sana Mhe. Mbunge kwa kutuletea mitungi hiyo Rafiki kwa mazingira, sasa tutapika kwa wakati mfupi . Tunakushukuru kwa kuwajali wananchi kata zote za Jimbo la Dodoma pamoja na taasisi mbalimbali za umma. Nendeni mkatumie mitungi hiyo ya kisasa ”,amesema Senyamule.
“Kati ya wabunge wanaofanya kazi vizuri, Mavunde yumo. Mavunde ni kijana mchapakazi na msikivu sana, mlifanya maamuzi sahihi kuchagua mbunge huyu. Naomba tumuunge mkono, tusimkatishe tamaa, tumtie moyo na tumuunge mkono kwa kumpa ushirikiano, huyu ni mtoto wetu tusitafute mtoto mwingine”,amesema Mhe. Senyamule.
“Hapa tulipo tunafanya kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, na Mbunge huyu anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo”,ameongeza.