Featured Kitaifa

DK.BITEKO ASISITIZA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA WATANZANIA WOTE

Written by mzalendoeditor
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko,akizungumza wakati wa uiznduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lililoenda sambamba  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa nishati safi ya kupikia siyo tu ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan bali ni ajenda ya kuokoa maisha ya watu.
Ameyasema hayo leo Septemba 13, 2024 jijini Dodoma wakati akizindua jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya kuwezesha miradi ya nishati safi ya kupikia.
“Naomba ajenda hii iwe ya watu wote, Serikali inafanya kila linalowezekana kushusha bei ya nishati safi ya kupikia na kuifanya nishati hiyo iweze kupatikana nchi nzima, imeanza kwa kutoa mitungi 400,000 itakayouzwa kwa bei ya ruzuku.” Amesema Dkt. Biteko.
Akizungumza kuhusu mikataba saba iliyosainiwa, Dkt. Biteko amesema imani ya wananchi ni kuona mikataba hiyo inafanyiwa kazi kwani ni aibu kwa Watanzania kushuhudia utiaji saini huo halafu wasione matokeo.
Aidha, ametoa agizo kwa Wizara ya Nishati na taasisi zake kuwa mfano kwa kuanza kutumia nishati ya umeme wa jua kwenye ofisi hizo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo amesema ushirikiano baina ya REA na Jeshi la Magereza umewezesha kuanzishwa kwa programu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia magerezani ambayo inatekelezwa katika vituo 211 vya jeshi hilo.
“Programu hii itawezesha upatikanaji wa chanzo kikuu na chanzo mbadala cha nishati safi ya kupikia ambapo gharama za mradi huu ni shilingi bilioni 35.2.” Amemalizia Sillo.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, kuwaamesema jengo hilo limejengwa ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhamia jijini Dodoma ambapo gharama za mradi huo ni shilingi bilioni 9.8.

Kuhusu mikataba ya Nishati Safi ya Kupikia alisema kwa upande wa Jeshi la Magereza,  mikataba iliyosainiwa ina thamani ya shilingi bilioni 35.23 ambapo kati ya fedha hizo 75.5% ambayo ni sawa na shilingi bilioni 26.57 zitatolewa na REA na 24.6% sawa na shilingi bilioni 8.66 zitatolewa na Jeshi hilo kwa mradi utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitatu katika Magereza 129 ya Tanzania Bara.

Mkataba wa Magereza unahusisha masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mifumo ya bayogesi (gesi vunde) 126, usimikaji wa mifumo 64 ya gesi ya LPG, usimikaji wa mfumo wa gesi asilia, usambazaji wa mitungi ya gesi (LPG) ya kilo 15 ikiwa na jiko la sahani mbili ipatayo 15,920 kwa watumishi wa Magereza na usambazaji wa tani 865 za mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe kutoka STAMICO.

Mhandisi saidy amesema  kwa upande wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mikataba iliyosainiwa ina thamani ya shilingi bilioni 5.75 ambapo kati ya fedha hizo asilimia 76 ambayo ni sawa na shilingi bilioni 4.37 itatolewa na REA na huku asilimia 24 sawa na shilingi bilioni 1.39 itatolewa na JKT.

Amesema  fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi katika Kambi 22 za JKT kwa muda wa miaka miwili itakayohusisha ujenzi wa mitambo 9 ya bayogesi, majiko 291 ya kutumia mkaa mbadala (makaa ya mawe na tungamotaka), ujenzi wa mifumo 180 ya kupikia inayotumia LPG na sufuria zake, ununuzi wa tani 110 za mkaa unaotokana na makaa ya mawe, ununuzi wa mashine 60 za kutengeneza mkaa mbadala na mafunzo kwa vijana wapatao 50,000.

Wadau wengine waliosaini mikataba ya Nishati Safi ya Kupikia ni kampuni zinazofanya biashara ya gesi ya mitungi ikiwemo Taifa Gas, Manjis, Oryx pamoja na Lake Oil ambapo wanasambaza mitungi ya gesi ya kupikia ipatayo 452,445  kwa bei ya ruzuku katika mikoa yote ya Tanzania Bara.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (kulia) akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA)lililopo jijini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko,akizungumza wakati wa uiznduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lililoenda sambamba  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lililoenda sambamba  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Daniel  Sillo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamuleakitoa salamu za Mkoa wake  wakati wa uzinduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REA), Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

 Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy,akielezea mkakati wa REA wakati wa uzinduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

 Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Uzalishaji Mali SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata,akiipongeza REA kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Katungu,,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko (hayupo pichani) ,akizungumza wakati wa uiznduzi wa  jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lililoenda sambamba  na utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia,hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy, na Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Uzalishaji Mali SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata  wakionesha mkataba wa ushirikiano wa  utekelezaji wa Nishati Safi ya Kupikia mara baada kuusaini.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy, na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza  (CPG) Jeremia  katungu  wakionesha mkataba wa ushirikiano wa  utekelezaji wa Nishati Safi ya Kupikia mara baada kuusaini.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko,akishuhudia utiaji saini wa mikataba sita ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kati ya REA na Jeshi la Magereza na Jeshi la kujenga Taifa (JKT),hafla iliyofanyika leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma.

NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko amesema Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kunakuwa na unafuu katika upatikanaji wa bidhaa za nishati safi ya kupikia ikiwemo mitungi ya gesi  ili kumwezesha kila mwananchi  kutumia nishati iliyo safi na salama.

Katika kutekeleza jitihada hizo, Serikali  imetoa ruzuku kwa mitungi ya gesi zaidi ya 400,000 itakayouzwa kwa nusu gharama ya awali ambayo inasambazwa katika mikoa yote Tanzania Bara huku zoezi hilo likiwa ni endelevu.

Dkt. Biteko amesema hayo tarehe 13 Septemba 2024 jijini Dodoma wakati wa hafla ya Kusainiwa mikataba ya ushirikiano ya utekelezaji wa Nishati Safi ya Kupikia yenye thamani ya shilingi bilioni 50.98 kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na taasisi sita ambazo ni Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Jeshi la Magereza (TPS) na Wasambazaji wa Gesi ya kupikia, hafla ambayo ilienda sambamba na uzinduzi wa jengo la REA.

“Namshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake yanayowezesha Sekta ya Nishati kuendeshwa kwa mafanikio ambayo yamepelekea leo hii tushuhudie hatua ikizidi kupigwa katika kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia unaolenga kuokoa maisha ya watanzania na pia kuiwezesha Wizara ya Nishati kutatua changamoto zinazojitokeza lengo likiwa ni kutoa huduma iliyo bora kwa wananchi.” Amesema Dkt. Biteko

Kuhusu mikataba hiyo ya Nishati Safi ya Kupikia, Dkt.Biteko ameiagiza REA na wadau kuhakikisha kuwa matokeo yanaonekana tena kwa uharaka akieleza kuwa “itakuwa aibu sana watanzania wanaona mikataba imesainiwa huku kukiwa hakuna matokeo, tusione kawaida kwa ndugu zetu kupoteza maisha kwa kutumia nishati isiyo safi, tuwaokoe kupitia miradi hii na tutumie kila fursa inayojitokeza.”

Amesisitiza kuwa, ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia ni ya wote na inalenga kuokoa maisha ya watanzania hivyo hivyo iwe ni kipaumbele cha watu wote.

Kuhusu usambazaji wa nishati vijijini ikiwemo umeme, ameipongeza Bodi ya REA kwa kusimamia ipasavyo miradi hiyo vijijini na kwa kuwahimiza wakandarasi kukamilisha kazi kwa wakati.

Akizungumzia jengo la REA alilolizindua, Dkt.Biteko amesema litawawezesha watumishi kutoa huduma kwa wananchi na kuwapongeza REA kwa kujenga jengo hilo la kisasa lenye ghorofa tano kwa gharama ya shilingi bilioni 9.8 kwa miezi 18 badala ya  shilingi bilioni 13 zilizopangwa awali.

Pamoja na kuipongeza REA kwa ujenzi wa jengo hilo la kisasa amewakumbusha kuwa, uwepo wa jengo wa jengo hilo lazima uende sambamba na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

“ Mimi naamini Jengo hili kweli ni muhimu lakini muhimu zaidi ni huduma kutoka kwenu kwenda kwa wananchi, kama tunasema kwamba tuna jengo zuri la ghorofa tano, halafu tukatoa huduma mbaya, jengo hili halitakuwa na maana yoyote hivyo uzuri wake uonekane kwenye huduma kuanzia sehemu ya mapokezi na wananchi watoke katika jengo hili wakiwa na furaha.” Amesisitiza Dkt. Biteko

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ameagiza Watendaji wa Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa majengo ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake yanafungwa mfumo wa umeme jua ikiwa ni kuonesha kwa vitendo matumizi ya nishati safi yenye gharama nafuu.

kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Daniel  Sillo amesema tukio hilo ni alama ya ushirikiano kati ya REA na Taasisi za Jeshi ambapo amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za dhati katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, udhibiti wa rasilimali za misitu na kutengeneza fursa za ajira kupitia Nishati Safi ya Kupikia.

Amesema kusainiwa kwa mikataba hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia na  utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) kuwa taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 ziache matumizi ya kuni na mkaa na kuanza  kutumia vyanzo vya Nishati safi ya Kupikia ikwemo gesi asilia, umeme, bayogesi na makaa ya mawe yaliyoboreshwa.

Amesema kwa sasa nishati inayotumika kupikia chakula cha Wafungwa na Mahabusu  ni kuni kwa asilimia  98 ambapo Jeshi hilo lilianza kutekeleza Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia kwa kuanza kutumia nishati safi kupitia  gesi asilia na mkaa mbadala hivyo  kusainiwa kwa mkataba huo kutawezesha Jeshi la Magereza kutumia nishati safi ya kupikia kwenye magereza yake.

Amesema kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani itahakikisha fedha zilizotengwa pamoja vifaa kwenye programu hiyo zinasimamiwa ipasavyo ili lengo tarajiwa lifikiwe na hii ikienda sambamba na utoaji wa mafunzo  kwa watumishi wa Jeshi ili waweze kuisimamia na kutunza miundombinu itakayofungwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa pongezi kwa REA kwa kukamilisha jengo kubwa la kisasa ambalo linaifaharisha Dodoma  na pia amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa kutoa sh.bilioni 214 kwa ajili ya shughuli za umeme mijini na vijijini ambapo mkoani Dodoma asilimia 92.2 ya vijiji  vimefikiwa na umeme huku kazi hiyo usambazaji umeme ikiendelea.

Pia amempongeza Rais, kwa miradi ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia uhamasishaji wa nishati hiyo na kueleza kuwa kasi ya kutumia nishati safi kwa wananchi inaongezeka.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kusainiwa kwa mikataba hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akizindua  mjadala wa kitaifa wa Nishati Safi ya kupikia na kutilia mkazo wakati akizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na kwamba Wizara ya Nishati ina wajibu wa kutekeleza agizo hilo na ndio maana taasisi yake ya REA  imesaini mikataba husika

Amesema Mikataba iliyosainiwa inahusisha masuala mbalimbali ikiwemo kufunga mifumo ya nishati safi  ya kupikia pamoja na usambazaji wa majiko na mitungi ya gesi  ipatayo laki nne ambayo inatolewa kwa bei ya ruzuku kwa wananchi hasa maeneo ya vijijini.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy alisema kuwa, Wakala huo kuhamia kwenye jengo lake kumewezesha kuokoa shilingi milioni 650 zilizokuwa zikitumika kwa mwaka kulipia kodi ya pango ambazo sasa zinaelekezwa kwenye maendeleo ya huduma zinazotolewa.

Kuhusu mikataba ya Nishati Safi ya Kupikia alisema kwa upande wa Jeshi la Magereza,  mikataba iliyosainiwa ina thamani ya shilingi bilioni 35.23 ambapo kati ya fedha hizo 75.5% ambayo ni sawa na shilingi bilioni 26.57 zitatolewa na REA na 24.6% sawa na shilingi bilioni 8.66 zitatolewa na Jeshi hilo kwa mradi utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitatu katika Magereza 129 ya Tanzania Bara.

Mkataba wa Magereza unahusisha masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mifumo ya bayogesi (gesi vunde) 126, usimikaji wa mifumo 64 ya gesi ya LPG, usimikaji wa mfumo wa gesi asilia, usambazaji wa mitungi ya gesi (LPG) ya kilo 15 ikiwa na jiko la sahani mbili ipatayo 15,920 kwa watumishi wa Magereza na usambazaji wa tani 865 za mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe kutoka STAMICO.

Mhandisi saidy alisema kwa upande wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mikataba iliyosainiwa ina thamani ya shilingi bilioni 5.75 ambapo kati ya fedha hizo asilimia 76 ambayo ni sawa na shilingi bilioni 4.37 itatolewa na REA na huku asilimia 24 sawa na shilingi bilioni 1.39 itatolewa na JKT.

Amesema  fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi katika Kambi 22 za JKT kwa muda wa miaka miwili itakayohusisha ujenzi wa mitambo 9 ya bayogesi, majiko 291 ya kutumia mkaa mbadala (makaa ya mawe na tungamotaka), ujenzi wa mifumo 180 ya kupikia inayotumia LPG na sufuria zake, ununuzi wa tani 110 za mkaa unaotokana na makaa ya mawe, ununuzi wa mashine 60 za kutengeneza mkaa mbadala na mafunzo kwa vijana wapatao 50,000.

Wadau wengine waliosaini mikataba ya Nishati Safi ya Kupikia ni kampuni zinazofanya biashara ya gesi ya mitungi ikiwemo Taifa Gas, Manjis, Oryx pamoja na Lake Oil ambapo wanasambaza mitungi ya gesi ya kupikia ipatayo 452,445  kwa bei ya ruzuku katika mikoa yote ya Tanzania Bara.

 

About the author

mzalendoeditor